NA SALVATORY NTANDU
Watu wasiojulikana wamemvamia na kumuua papo hapo Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyambula kata ya Ngongwa, Halmashauri ya mji wa Kahama Hamisi Kadilanha Salehe(58) kwa kumkata na kitu chenye ncha kali wakati akiwa amelala na mkewe Shija Mkela Maziku(45).
kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema kuwa,tukio hilo jana majira ya saa mbili usiku ambapo watu hao walitekeleza mauaji hayo na kisha kumjeruhi shija Mkela Maziku.
Amesema chanzo cha tukio hilo kinasadikiwa ni imani za kishirikina kutokana na tukio la kupigwa na radi mwezi wa Februari mwaka huu ambapo ilisababisha kifo cha mdogo wake na marehemu Mhoja Kadilanha Salehe(45) na mkewe Pili Tabu Mabula(36)na wengine waliokuwa nao hawakupata madhara kutokana na radi hiyo.
Amefafanua mbinu iliyotumika ni kuvunja mlango na kumvamia akiwa amelala chumbani kwake na mkewe nakuongeza mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Halmashauri Mji wa Kahama.
Kamanda Abwao amesema katika tukio hilo watu waliwajeruhi watu wawili ambao ni mke wa marehemu Shija Maziku na Dada yake Pili tabu Mabula ambao wote wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Halmashauri ya mji.
Ameongeza kuwa jeshi la polisi kwa kushirikina na wananchi linaendelea kuwatafuta watu hao walifanya mauji na watakapobainika watachukuliwa hatua za kisheria kama ambavyo wamekuwa wakichukuliwa watu wengine wanaojichulia sheria Mkononi.
Post a Comment