Mwenyekiti wa Halmshuri y Wilaya ya Bukoba Hashimu Murshid Ngeze akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu wanafunzi kutokatishwa tamaa na wazazi na walezi Mkoani Kagera. (PICHA NA LYDIA LUGAKILA, KAGERA)
Na Lydia Lugakila Kagera.
Wazazi na walezi mkoani Kagera wametakiwa kuacha dhana potofu ya kuwavunja moyo watoto wao hasa wanafunzi wanapokaribia kufanya mitihani yao ya taifa kwa kuwatamkia neno FANYA VIBAYA MTIHANI ILI UWEZE KUSHINDWA.
Kauli hiyo imetolewa leo septemba 3, 2019 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Murshid Hashimu Ngeze katika kuelekea kufanya mitihani ya Taifa kwa wanafunzi wa shule ya msingi kote nchini.
Ngeze Amesema kuwa kitendo hicho cha mzazi au mlezi kumtamkia mwanaye kuwa afanye vibaya mtihani ili ashindwe ni kikwazo kikubwa kinachokwamisha juhudi na ndoto za mtoto katika kufikia malengo yake tarajiwa.
‘’Si vizuri mtoto usimvunje moyo mwache mtoto afanye vizuri njia ya jinsi mtoto atasoma ni mungu anayejua sisi Halmashauri tupo tunajua ni jinsi gani mtoto atapata Elimu amesema.’
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kutoongea na watoto wao hasa mabinti katika misingi iliyo bora, hivyo amewahimza wazazi na walezi kununua vifaa muhimu vya watoto ili kunufaika na Elimu bure iliyoko hapa nchini.
Amesema ni muhimu sana wazazi na walezi kukaa na watoto wao wa kike kuwafundisha jema na baya ili waweze kukua ki maadili
Katika hatua nyingine Ngeze Amekemea tabia za baadhi ya Madreva wa pikipiki marufu kama boda boda wanaowadanganya wanafunzi kwa kuwarubuni kwa zawadi na lifti, kuwa tabia hiyo sio nzuri ambapo tayari mikakati mbali mbali inafanyika ili kupambana na vitendo hivyo.
Ambavyo huwafanya wanafunzi kukatisha masomo kwa kupata ujauzito na kushindwa kufikia malengo yao
Amewataka wanafunzi wilayani humo kufanya mtihani wao vizuri unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo Septemba kumi na moja na kumi na mbili mwaka huu bila kuwa na vikwazo vya kusingizia kufuata shule umbali mrefu kwani tayari ujenzi wa shule unaendelea wilayani humo .
Aidha ametoa toa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzani Dokta John Magufuli kwa kitendo cha kuwaita ikulu watendaji wa kata kote nchini kwa lengo la kuzungumza nao kwa kuwapa maelekezo ya kuijenga nchi.
Akigusia sualala maendeleo amesema kuwa katika utawala wa Rais Magufuli vijiji 94 katika halmashauri hiyo kila mwaka kijiji kimoja kitakuwa kinapata elfu 45 katika uendeshaji wa maendeleo kwenye vijiji hivyo.
Ametaja hatua hiyo kubwa ni kutokana na juhudi za Rais Magufuli na kudai kuwa halmashauri hiyo haijawahi kugusa fedha za maendeleo na kuziweka katika shughuli za kawaida
Ikumbukwe kuwa Halmashauri hiyo ina kata 29 vijiji 94 na katika vijiji vyote hivyo vina miradi mbali mbali inayoendelea miradi hii ipo katika makundi matatu ambayo ni miradi ya serikali kuu, miradi ambayo inatoa fedha kutoka mapato ya ndani na miradi ambayo ni ya wahisani kwa ushirikiano na wananchi.
Mwenyekiti huyo amewataka wananchi kushiriki katika miradi mbali mbali ya kimaendeleo kwa ukamlifu na kuguswa na miradi hiyo ambapo hadi sasa ameitaja Halmashauri hiyo kuwa katika hatua nzuri kwani miradi mingi inaendelea kutekelezwa ambapo usimamizi wa fedha ni mzuri pia.
Hata hivyo amesema kuwa serikali hutumia fedha nyingi katika miradi ya maendeleo kwa wananchi hivyo ni vema miradi hiyo itunzwe na kulindwa.
Na kuwataka wananchi kutoa taarifa mara moja pale wanapogundua au kubaini baadhi ya watu wanaohujumu miradi hiyo ili hatua kali ichukuliwe.
Taarifa za ukaguzi mbali mbali zimekuwa zikifanyika ikiwemo ya CAG au ukaguzi wa ndani kutoka mkoani ambapo mara nyingi wamekuwa wakiikagua na pale ambapo wamekuwa wakikuta mapungufuwamekuwa wakishauri na mwisho nitumie fulsa hii kwaniaba yangu na kwaniaba ya wananchi wangu kumpongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC.
Post a Comment