Naibu waziri wa Kilimo Mhe.Husein Bashe amesema moja ya vikwazo vilivyokuwa vinasababisha Sekta ya Kilimo kuendelea kuwa na Matatizo ni pamoja na Migogoro na kesi za muda mrefu dhidi ya Makampuni za Kilimo ambapo serikali imedhamiria kufuta kesi zote zilizokuwa zinazikabili kampuni hizo ili ziweze kununua Mazao ya wakulima.
Mhe.Bashe amesema ameyasema hayo Sept.3,2019 jijini Dodoma katika mkutano uliokutanisha wizara ya Kilimo,Wizara ya Viwanda na biashara,Wizara ya Fedha pamoja na wadau wa kilimo hapa nchini.
Naibu Waziri Bashe amesema kampuni za kilimo zilikuwa zikidaiwa zaidi ya Tsh.Trilioni 10 na Serikali hali ambayo ilikuwa inasababisha kushindwa kwenda kutoa huduma kwa wakulima hivyo serikali ina mkakati kabambe wa kufuta kesi na faini zote hizo ili ziweze kutoa huduma kwa wakulima.
Aidha,Mhe.Bashe amesema wamekubaliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania[TRA] kuwa ndani ya siku 90 Kuanzia leo Sept.4,2019 suala la madai kwa kwa Kampuni 4 za kilimo limekuwa limeisha ili kampuni hizo ziendelee kununua mazao kwa wakulima.
Pia Naibu Waziri Bashe amesema kuna zaidi ya kilo Mil.12 za Tumbaku zipo mikononi mwa Wakulima na Kampuni za kilimo chini ya Bodi ya Tumbaku Tanzania zitakutana na wakulima kununua kilo hizo kuanzia Sept.12,2019 .
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku ,Tanzania Tobacco Board[TTB] Hassan Mwakasuvi amesema ni vyema wakulima kuheshimu mikataba huku akisema kuwa maazimio ya kikao hicho ni Faraja kwa wakulima katika msimu ujao wa kilimo.
Naye Mwenyekiti wa vyama vikuu vya wakulima wa Tumbaku Tanzania Emanuel Cherehani ameishukuru serikali kwa maamuzi hayo huku akiomba kuanza kutekelezwa ndani ya Muda husika uliotajwa ili isiathiri zaidi wakulima huku akiwaomba wakulima kuendelea kutunza mazao yao ya tumbaku.
Aidha,Cherehani amesema hapo awali uzalishaji wa zao la tumbaku kwa mwaka 2015 ilikuwa milioni 120 lakini umeshuka mpaka milioni 41 jambo ambalo limeathiri kwa wakulima na Serikali kwa Ujumla.
Post a Comment