Featured

    Featured Posts

CRDB BANK YAPATA FAIDA KUBWA SHILINGI BILIONI 92

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam, kuhusu mafanikio ya benki hiyo.

Na Richard Mwaikenda


BENKI ya CRDB imefanikiwa kupata faida kubwa ya Bil. 92 baada ya kodi  kwa kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka huu.

Mafanikio hayo yametangazwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela katika mkutano na waandishi wa habari, kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.

Nsekela amesema kuwa hayo ni mafanikio makubwa ambayo ni sawa na asilimia 76 na kwamba  kwa kipindi kama hicho mwaka jana, walipata faida sh. Bil. 52.

Ametaja siri ya mafanikio hayo kuwa ni kuwa ni ufanisi , utendaji na uwajibikaji wa imu nzima ya wafanyakazi, kuwa karibu na wateja ambao amana zao hadi sasa imefikia Sh. Trilioni 4.8 hivyo kuongoza mabenki mengineTanzania.

Alitaja zingine kuwa ni; kuwajali wateja, kuboresha huduma na kuongeza wigo wa kutoa mikopo kwa wateja yenye  riba nafuu zinazoanzia asilimia 14.5, 15, 17, na 18 hali inayochochea wateja wengi kujiunga na benki hiyo.

Nsekela amesema kuwa jambo lingine linaloifanya benki hiyo kuzidi kuwa kinara nchini ni  kuwajali wateja kwa kuwasogezea huduma kwa kusajili mawakala ambapo hadi sasa benki hiyo ina mawakala  11,612 nchi nzima. Ina matawi 240, ATM 551,  na vituo vya mauzo (POS),2400 2400

Jambo lingine alilolitaja kuwa linaongeza ufanisi wa benki hiyo ni ubunifu, kwani hivi karibuni ameanzisha dawati maalumu la kuwa hudumia wanawake kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu ikiwemo kuwaidhinishia mikopo bila kuwa na dhamana, wakitambua wengi wao hawana dhamana.

Pia masuala ya dijitali yamechangia kwa aslimia kubwa wateja kuwa karibu na benki hiyo kwani hujihudumia popote walipo kwa kutoa fedha kupitia simu banking kwa kutumia mitandao mbalimbali ya simu.


 Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari, kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 Baadhi ya watendaji wa CRDB wakiwa katika mkutano huo

 Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakisikiliza kwa makini wa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo akielezea kuhusu mafanikio ya benki hiyo


  Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa akiruhusu wanahabari kuuliza maswali kwa MD Nsekela wakati wa mkutano huo..
MD Nsekela akipongezwa na wafanyakazi baada ya kumaliza kuzungumza na wanahabari kuhusu utendaji mzuri wa benki hiyo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana