Na.Vero Ignatus,Arusha.
Hatimaye mwili wa nahodha wa mtumbwi Samwel mhina (29)aliyezama kwa dhoruba ya upepo katika ziwa Momela mkoani Arusha siku nne zilizopita umepatikana.
Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha ACP Koka Moita amethibitisha kupatikana kwa mwili wa marehemu Samwel Gelda Mhina akiwa ameshafariki.
"Kwa kushirikiana na Jeshi la uokoaji na zimamaoto tumefanikiwa tumefanikiwa kuupata mwili wa marehemu Samwel Gelda Mhina,akiwa ameshafariki tayari" alisema Kamanda Moita.
Mkuu huyo wa wilaya ya Arumeru ametoa pole kwa familia na kusema kuwa huo ni msiba mzito,ambapo serikali ya awamu ya tano imefanya kila jitihada na ndani ya siku nne mwili huo umeweza kupatikana.
“Hili lilikuwa ni hitaji la ndugu wa samweli kwamba wanahitajika wawepo wazamiaji na sisi tulifanya kila jitihada za kuwapata wazamiaji kutoka dare s salaam waliingia jana na leo alfajiri tukaanza zoezi na ndani ya saa moja, tukadfanikiwa kuupata mwili wa Samweli akiwa ameshafariki.”alisema Jerry
Murro ametoa wito kwa jamii wasisubirie matukio yatokee ndipo wachukue tahadhari,bali amewataka kuchukua tahadhari wakati wowote,.
" Wazamiaji waliangalia chini zaidi kuona kama kuna mtu mwingine yeyote aliyekwama ziwani kwa bahati mbaya,kwa taarifa walizotupatia ni kwamba hakuna mtu mwingine anayehofiwa kuwa katika zile ziwa dogo la momela"alisema Murro.
Dedis Samwel Mhina ni baba mdogo wa marehemu wameishukuru serikali kwa kuwasaidia kuupata mwili wa ndugu yao,mwili umehifadhiwa katika hospital ya Mount Meru,taratibu za mazishi zitakapokamilika wanatarajia kumzika ndugu yao mkoani Tanga.
Ikumbukwe kuwa tukio hilo la kuzama kwa mtubwi lilitokea majira ya saa 8:45 mchana oktoba 1,2019 katika kijiji cha Olkungwando,kitongoji cha Momela ,kata Ngarenanyuki,tarafa ya King'ori wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.
Mtalii Rosenbever Heike alifanikiwa kujiokoa kwa kuogelea ,nahodha Samwel Mhina akazama ziwani ambapo mwili wake umeoatikana leo octoba 4,2019 akiwa amefariki.
Post a Comment