Featured

    Featured Posts

MATEMBEZI YA ARUBAINI YA IMM HUSSEIN AS, MJUMUIKO KWA AJILI YA UHURU NA KUWATETEA WALIODHULUMIWA

Akizungumza Ijumaa, Shamkhani alisisitiza kuwa: "Katika Arubaini ya mwaka huu, mamilioni ya wafanyaziara kutoka Iran na nchi zingine duniani wanashiriki katika mjumuiko mkubwa wa Arubaini huku kukiwa na usalama Iran na Iraq."
Matembezi makubwa ya Arubaini ni mjumuiko uliojaa thamani za kimaanawi na itikadi za kidini na wakati huo huo una ujumbe kwa dunia.
Matembezi ya Arubaini yana sifa kadhaa za kipekee na thamani takasifu kama vile kujitolea muhanga waumini katika kuhudumiana na pia ni madhihirisho ya ukarimu.
Kaitka hali ambayo hivi sasa eneo la Asia Magharibi linashuhudia matukio nyeti ya kisiasa, Arubaini ni fursa ya kuupa sura ya kimataifa mwamko wa Ashura katika mhimili wa mapambano dhidi ya dhulma na kusimama kidete kukabiliana na madhalimu.
Pamoja na kuwa tukio la Arubaini kimsingi linawahusu Waislamu lakini tunashuhudia namna ambavyo wafuasi wa dini nyinginezo, hasa Wakristo na Mayahudi wanavyojumuika katika matembezi ya Arubaini. Nukta hii inaashiria ukweli huu kuwa, harakati na fikra ya Imam Hussein AS ya kutetea uhuru na uadilifu si ya Mashia na Waislamu pekee.
Kama alivyosema Admeri Ali Shamkani: "Kujumuika idadi kubwa ya watu katika matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS ni jambo linaloonyesha kuwa, ujumbe wa kiutamaduni wa Arubaini hauishii Karbala na Bein al Haramein pekee."
Ayatullah Mohsen Ghoroyan, msomi maarufu katika vyuo vya kidini vya Qum ameashiria umuhimu na nafasi ya kipekee ya matembezi adhimu ya Arubaini na kusema: "Katika mlingano wa dunia, mjumuiko mkubwa wa waombolezaji wa Imam Hussein AS unazingatiwa na unapewa umuhimu kimataifa; hii ni kwa sababu wachambuzi wa masuala ya kisiasa duniani wanafahamu kuwa wakati mapenzi kwa Aba Abdillah (Imam Hussein AS)  yanaleta mjumuiko mkubwa kama huu, basi watu waliojumuika wanaweza kukusanyika kwingineko na kubadilisha mlingano wa kimaada.
Mjumuiko wa Arubaini ya Imam Hussein AS mjini Karbala
Ni kwa kuzigatia mtazamo huo ndio maana matembezi ya Arubaini mbali na kuwa na thamani za kidini na kimaanawi pia yana taathira za kina za kisiasa na kijamii.
Matembezi haya yanafungamana na historia na sasa yamebadilika kuwa nukta ya pamoja ya maelewano baina ya Waislamu na ni rasilimali ya kijamii na kwa hakika ni dhihirisho la nguvu laini ya Waislamu.
Kwa mtazamo wa Ă‰mile Durkheim mtalamu maarufu wa masuala ya kijamii kutoka Ufaransa, kile ambacho kinapelekea jamii iendelee kusimama imara ni 'hisia za daima' miongoni mwa walio katika jamii." Durkheim anaamini kuwa: "Kila jamii inaona ulazima wa kuwa na safu zilozojipanga kwa nidhamu, kuwa na hisia na malengo ya pamoja ambayo yataihifadhi jamii hiyo na kuiunganisha. Hii ni kwa sababu hizo ni nukta ambazo huleta umoja na utambulisho wa jamii."
Hivi sasa mjumuiko adhimu wa Arubaini umeweza kuwa na taathira kubwa na chanya katika kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa mamilioni waliofika Karbala kutoka maeneo mbali mbali ya dunia.
Tabaan, pembizoni mwa fursa kama hizo kuna vitisho pia dhidi ya matembezi adhimu ya Arubaini. Kuna njama za kuvuruga usalama, hasa hujuma za kigaidi na njama zinginezo za ajinabi waliojipenyeza ili kuibua taharuki katika matembezi hayo adhimu ili hatimaye kuyadhoofisha. Lakini  hata pamoja na kuwepo vitisho, hatari na matatizo mengine mengi, matembezi ya Arubaini yanafanyika kwa mapenzi na kujitolea kwa wafanyaziara. Uzoefu wa mwaka huu na miaka iliyopita unaonyesha kuwa,kufanyika kwa mafanikio matembezi ya Arubaini kunatokana na thamani zake za kipekee.
Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akizungumza siku chache zilizopita katika hafla ya wanachuo wa kijeshi waliohitimu katika Chuo cha Imam Hussein AS  cha Maafisa wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema,  wakati wa kudhihiri kwake katika historia ya Uislamu, Arubaini ilikuwa 'chombo cha habari chenye nguvu cha tukio la Ashura'. Aidha alisisitiza kuhusu kuenea na kukita mizizi umaanawi, fikra na maarifa katika matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein  AS na kuongeza kuwa,  wenye busara na wasomi  wanapaswa kufanya kazi na jitihada katika maudhui hii.


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana