Tunduru 30, Oktoba 2019.Ofsi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma inapenda kukanusha habari ya upotoshaji iliyotolewa na Gazeti la HabariLeo la tarehe 28 Oktoba 2019 na Kituo cha Televisheni cha ITV ikisomeka kuwa “Wanafunzi 350 waacha shule kwa utoro, mimba,” habari hii haina ukweli wowote kama ilivyoripotiwa.
Tunapenda kuuarifu umma kuwa baada ya kuwepo kwa taarifa hiyo Ofsi yaMkurugenzi imefanya ufuatiliaji wa kina katika Shule ya Sekondari Marumba ambayo imetajwa katika habari hiyo iliyosema kuwa wanafunzi 350 wa shule hiyo wameshindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya utoro na mimba kwa kipindi cha miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2016 hadi 2019.Ni vyema umma ukafahamu kuwa katika kipindi cha miaka minne yaani 2016 hadi 2019, shule hii ilipangiwa idadi ya wanafunzi 603 ikiwa wavulana320 na wasichana 283, waliosajiliwa kwa kipindi hicho ni wanafunzi 515 ikiwapungufu ya wanafunzi 88 kati ya waliopangwa.
Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wanafunzi waliopo katika shule ya Sekondari Marumba hadi kuanzia tarehe 28/10/2019 ni 345 ikiwa wavulana208 na wasichana 137 kukiwa na upungufu wa wanafunzi 170. Akitoa ufafanuzi huo Mkurugenzi Mtendaji Halmasahuri ya Tunduru Gasper Balyomi amesema hii ni wazi kuwa idadi ya wanafunzi 350 wa sekondari yaMarumba walioripotiwa hawajulikani walipo hazina ukweli wowote kufuatia takwimu zilizotolewa na kubaini kuwa:-1. Kwa kipindi cha miaka minne mfululizo jumla ya wanafunzi 20 walihama kwenda katika shule nyingine
2. Wanafunzi 15 waliacha masomo baada ya kupata ujauzito 3. Wanafunzi 63 waliacha masomo kutokana na sababu mbalimbali 4. Wanafunzi 72 waliopewa nafasi ya kurudia masomo baada ya kufelikidato cha pili baadhi yao wazazi waliamua kuwapeleka katika vyuovya Ufundi stadi kama (VETA) na shule binafsi.Hivyo kufanya jumla ya wanafunzi 170 kwa kipindi cha miaka minne ndiohawapo shuleni tofauti na taarifa ilivyoonesha jumla ya wanafunzi 350 washule hiyo wameacha masomo.Aidha kuhusu suala la utoro wa reja reja Halmshauri inaendelea kushirikianana wazazi pamoja walezi wa wanafunzi katika kuahikisha utoro mashuleniunadhibitiwa. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Tunduru
Post a Comment