Featured

    Featured Posts

WANANCHI SALASALA WAMTUMA DC CHONGOLO KUFIKISHA UJUMBE WAO KWA RAIS DK.MAGUFULI


*Wachekelea kupata maji safi na salama ya bomba, Kilimahewa nako yanukia 

Na Said Mwishehe, Michuzi Blog

WANANCHI wa Salasala Juu wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam  wamemtuma Mkuu wa Wilaya hiyo Daniel Chongolo kufikisha ujumbe wao 
shukrani zao za dhati kwa Rais Dkt.John  Pombe Magufuli baada ya changamoto ya kukosa  maji kwa muda mrefu kupata ufumbuzi.

Kwa mujibu wa wananchi hao ni kwamba pamoja na kuwepo kwa changamoto nyingine lakini kukosekana kwa maji ilikuwa kero na ilisababisha mateso makubwa kwao lakini wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na hasa Rais Magufuli kwa kutatua kero hiyo.

Wananchi hao wamesema kupata maji safi na salama kwao ilikuwa ni ndoto ya miaka mingi hatimaye chini ya utawala wa Rais Magufuli nao wameonja ladha ya maji ya bomba baada ya Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) kukamilisha mradi wa kusambaza maji katika eneo hilo la Salasala Juu.

Akizungumza leo Oktoba 30, 2019 baada ya kuzindua rasmi maji ya bomba, 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amewaaambia wananchi hao wa Salasala Juu kwamba Serikali ya Rais Magufuli imeamua kumtua ndoo mwanamke kichwani na hivyo imedhamiria kutatua changamoto ya upatikanaji maji katika Wilaya hiyo na maeneo mengine.

Wakati Chongolo anazungumza na wananchi hao, wengi wao walionekana wenye furaha kubwa kwa kupata maji ambapo baadhi yao walisikika wakieleza waziwazi kufurahishwa na utawala wa Rais Magufuli ambao umeamua kujikita kutatua kero za wananchi.

" Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kumtua mama ndio kichwani katika Jiji la Dar es Salaam. Katika kutatua changamoto ya uhaba wa maji kuna maeneo ambayo yamepewa kipaumbele na hasa maeneo yenye muinuko ambayo maji hayafiki kwa uraihisi.

"Hivyo DAWASA ilianza kwa kuweka miundombinu ikiwemo kujenga matenki ya kuhifadhi maji matano ambayo manne yanauwezo kuhifadhi lita milioni sita na moja linauwezo wa kuhifadhi lita milioni tano.Hivyo niwahakikishie wananchi tuna uhakika wa maji ya kutosha na ya uhakika na hii yote imewezekana chini ya Rais Magufuli ambaye ameamua kutoa Sh.bilioni 72 kutatua changamoto ya maji,"amesema Chongolo.

"Uwekezaji wa Sh.bilioni 72 ndugu zangu wananchi si mdogo lakini Rais wetu kwa mapenzi mema aliyonayo kwetu ameamua kutoa fedha hizi kuhakikisha tunatatua changamoto ya maji na kwa Kinondoni nina uhakika ukosefu wa maji itabaki kuwa historia ili tuanze kushughulika na mambo mengine,"amesema Chongolo.

Mbali ya kutatua changamoto ya maji Salasala, Chongolo pia amepata nafasi ya kwenda kuzungumza na wananchi wa Kilimahewa ambako nako tayari 
usambazaji wa mabomba umeanza kutekelezwa kwa lengo hilo hilo la kutatua kero ya ukosefu wa maji ndani ya Wilaya ya Kinondoni ambapo amewahakikishia wananchi kuwa mradi huo utamfikia kila mtu.

"Tunaendelea kutatua changamoto ya maji, niwaombe wananchi hakikisheni mnajiandikisha kuomba kuwekewa maji, pili miundombinu ya maji ambayo inasambwaza ilindeni kama mboni ya jicho.Mkiona mtu anaharibu miundombinu hii toeni taarifa na atakeyabainika kuharibu hana tofauti na mhujumu uchumi,"amesema Chongolo wakati anazungumza na wananchi wa Kilimahewa.

Hata hivyo amesema Dawasa wanafanya kazi kubwa ya kusambaza miundombinu ya maji na wataendelea na kazi hiyo bila kuchoka, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi.

Kuhusu gharama ya bei ya ndoo ya maji, amesema haizidi Sh.35 wakati hivi sasa wananchi wananunua ndoo ya maji hadi Sh.500, hivyo ni vema ikafahamika dhamira ya Serikali ni kuona maji yanapatikana kwa uhakika na gharama nafuu maana sio biashara bali ni hitaji muhimu

Mkazi wa Salasala Juu Ashura Suleiman na mkazi  Bakari Joshua wa 
Kilimahewa wamesema Rais Magufuli kwa mambo anayoyafanya 
amethibitisha yeye ni Rais wa wanyognge, hivyo watamuunga mkono kwa kila jambo la maendeleo analofanya kwa ajili ya Watanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akimtwisha ndoo  Ashura Seleman wakati wa uzinduzi rasmi wa maji ya bomba ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) eneo la Salasala Juu  wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kulia ni Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Tegeta Philemon Boniface.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wa Salasala Juu mara baada ya kuzindua bomba la maji ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Tegeta Philemon Boniface (katikati) akitoa ufafanuizi wa kutandaza mabomba ya DAWASA katika eneo la Kilimahewa Juu wakati Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo alipofanya ziara maeneo hayo ambayo yalikuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa muda mrefu,katika wilaya hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Boko, Mhandisi Felchesm Kimaro.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza jambo na Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Tegeta Philemon Boniface(katikati) pamoja na Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Boko Mhandisi Felchesm Kimaro wakati wa ziara ya kukagua miundo mbinu ya Maji kwa wananchi wa eneo hilo.Picha na Michuzi JR (MMG).

Baadhi ya mambomba yatakayotandikwa kwenye eneo la Kilimahewa Juu lililokuwa na tatizo kubwa ya upatikanaji wa maji wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wa eneo la Kilimahewa Juu mara baada ya kufanya ukaguzi wa mabomba yatakayotandikwa kwenye eneo hilo ili kuweza kupata maji ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA),wakati wa ziara hiyo. Wa kwanza kushoto ni  Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Tegeta Mhandisi Philemon Boniface na kulia ni  Meneja wa DAWASA Mkoa wa Kihuduma Boko Mhandisi Felchesm Kimaro.Picha na Michuzi JR (MMG).
Baadhi ya wananchi wa Kilimahewa Juu wakimsilikiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo alipofanya ziara kwenye miundombinu ya maji ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ili kuweza kujionea na kuhakikisha maji yanawafikia wananchi hao.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akichimba mtaro kwa ajili ya kupitisha mabomba ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ili wananchi wa Kilimahewa Juu kupata maji safi. Picha na Michuzi JR (MMG).
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana