Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na gazeti la Washington Post kwa ushirikiano na kanali ya televisheni ya ABC yanaonesha kuwa, asilimia 58 ya Wamarekani waliotimiza masharti ya kupiga kura wanachukizwa na mtindo wa uongozi wa Trump kwa ujumla, huku asilimia 66 wakisema kuwa mwanasiasa huyo hajaendesha nchi kwa hadhi na shakhsia ya rais.
Aidha utafiti huo unaonesha kuwa, asilimia 54 ya wananchi wa Marekani wanaamini kuwa sera ghalati za Trump zimeifanya nchi hiyo ipoteze heshima yake katika uga wa kimataifa.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, asilimia 60 ya Wamarekani wamesema kuwa Trump sio mtu wa kuaminika na mwenye muamana, hana haiba ya kuwa rais na wala haelewi changatmoto na matatizo yanayowakumba wananchi wa kawaida.
Takwimu na chunguzi mbalimbali za maoni zinaonyesha kuwa, Donald Trump amezidi kupoteza hali ya kuaminiwa siku baada ya siku ndani na nje ya nchio.
Septemba mwaka huu, televisheni ya CNN iliripoti kuwa Trump ametoa madai ya uongo mara 27 kupitia hotuba yake iliyochukua muda wa dakika 95.
Post a Comment