Featured

    Featured Posts

MAFURIKO YAMEUA WATU 17 SOMALIA, 370,000 WAACHWA BILA MAKAZI

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA) imesema watu wasiopungua 17 wameaga dunia baada ya kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Somalia.
Taarifa iliyotolewa jana Jumatano na OCHA imesema watu zaidi ya 370,000 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na athari za mvua na mafuriko hayo katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika hususan katika wilaya ya Belet Weyne.
Taasisi hiyo ya UN imebainisha kuwa, maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo ni majimbo ya Hirshabelle, Jubaland na Kusini Magharibi, ambapo mashamba ya kilimo, miundombinu na mabarabara yameharibiwa na majanga hayo ya kimaumbile.
Haya yanajiri siku chache baada ya watu wengine 15 kupoteza maisha katika ajali ya kuzama boti katika mji wa Beledweyn katikati ya Somalia. 
Mafuriko nchini Somalia
Wakati huohuo, Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema kuwa linahitaji msaada wa dola milioni 10 za Marekani ili kukidhi mahitaji ya dharura ya watoto walioathiriwa na mafuriko nchini Sudan Kusini. Mjumbe wa UNICEF nchini humo Mohamed  Ayoya amesema, zaidi ya watu laki 9 wakiwemo watoto 490,000 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.
Nchini Tanzania idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mvua inakadiriwa kuwa 40 na katika nchi jirani ya Kenya watu takribani 30 nao pia wamepoteza maisha kufuatia mafuriko. Watabiri wa hali ya hewa wanatarajia mvua hizo kubwa zitaendelea kunyesha hadi mwezi Disemba.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana