Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara amevitaka Vyama vya Siasa vya Upinzani viache kuchukua maamuzi ya ajabu ya kususia uchaguzi badala yake vidai haki kwa njia sahihi.
Akiwa bungeni leo Waitara amevitaka vyama vya siasa vya upinzani viache kuchukua maamuzi ya ajabu ya kususia uchaguzi badala yake vidai haki kwa njia sahihi.
Pia ametoa maagizo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kujipanga vyema ili kuvidhibiti vyama vya upinzani vilivyojipanga kufanya fujo nchini.
Amesisitiza kwamba kususa haijawahi kuwa njia sahihi ya kudai haki, na pia wale wote waliopanga kufanya fujo wajiandae kukutana na mkono wa chuma na wasije kuilaumu serikali kwa kitakachowakuta.
"Kama wewe umesusa kaa kimya waache wenzako wanaojua maana ya demokrasia wafanye uchaguzi" amesema.
Ikumbukwe hapo jana Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe alitangaza kuwa chama hicho kimejitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huul.

Post a Comment