Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aliyemaliza muda wake, Profesa Mussa Assad amesema kuwa, hakujua na wala hakuwahi kufikiri kama angeweza kutengeneza uadui wakati wa utekelezaji wa majukumu yake akiwa katika ofisi hiyo.
Kwa mujibu wa Profesa Assad, huenda waliotengeneza uadui dhidi yake ni kundi la watumishi waliokuwa wanakwenda kinyume na misingi ya kazi. “Sijawahi hata siku moja kufikiria kama ninatengeza uadui, inawezekana kuna watu niliwakwaza lakini ni kwa sababu ya kutosimamia misingi yao ya kazi.” Amesema. Professa Assad ameyasema hayo leo na kusisitiza kuwa, amewasamehe wale wote aliokwazana nao wakati alipokuwa akitekeleza majukumu yake akiwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Assad alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa walioshiriki Kongamano la sita la Taasisi za Kifedha za Kiislamu Barani Afrika lililofanyika leo Jumatatu Jijini Dar es Salaam. Hata mtaalamu huyo wa masuala ya mahesabu hakutaka kuzungumzia chochote kuhusu changamoto za ofisi hiyo, uteuzi wa anayerithi mikoba yake, wala kugusia tofauti zake na muhimili wa Bunge. Wakati huo huo Rais John Magufuli wa nchi hiyo amempa ujumbe mzito Charles Kichere, aliyeteuliwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Rais Magufuli amempa ujumbe huo baada ya kumwampisha Kichere na kumtaka atelekeze maagizo atakayopewa na mihimili mingine.
Post a Comment