Shehena ya Vyavu haramu aina na Makokoro vilivyokamatwa katika Operesheni inayoendelea katika vijiji vinavyolizunguka bwawa la Nyumba ya Mungu vikiwa tayari kwa kuteketezwa kwa moto.
Na.Vero Ignatus,Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Thomas Apson,ameteketeza kwa moto nyavu aina ya makokoro na vyandarua vya kujikinga na mbu, vinavyotumika kwa uvuvi haramu vilivyokamatwa katika oparesheni inayoendelea katika vijiji vinavyolizunguka bwawa la Nyumba ya Mungu vyenye thamani vya shs.39.3mil.
Apson amesema kuwa katika oparesheni hiyo wavuvi haramu 14 katika bwawa hilo wametiwa mbaroni kwa kuwatishia polisi wenye silaha waliokuwa doria na kuwataka waweke silaha ili wazichape ngumi kavu kavu.
Afisa Tarafa ya Lembeni Gikila Salisali amesema, baadhi ya watumishi wa umma wasiokuwa waaminifu wamekuwa kikwazo katika vita hivyo kwa wanashirikiana na wavuvi haramu na kuiomba serikali iwape boti ili kuimarisha doria ndani ya bwawa.
Wananchi wa vijiji hivyo bi Eda Eliakimu na bakari kingazi wakazi wa nyumba ya Mungu wameipongeza serikali kwa kutangaza upya vita hivyo ambavyo wamesema vinaweza kusaidia kupunguza kasi ya uvuvi haramu ambao umekuwa tishio kwa samaki wachanga ambao wangeweza kubadili maisha yao.
Post a Comment