Featured

    Featured Posts

WAKAZI WA KIGWA KUPATA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWA GHARAMA YA BILIONI 10


SERIKALI imeamua kupeleka maji katika Kata ya Kigwa wilayani Uyui kupitia mradi wa ujenzi wa bomba la maji kutoka Ziwa Victoria kwa gharama isiyopungua shilingi bilioni 10.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa baada ya kusikia kilio cha wakazi wa Kigwa cha tatizo la maji akiwa katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi.

Alisema kuwa eneo hilo hakuna mto wala bwawa na ndio maana katika kata hiyo kuna tatizo kubwa la maji na ndio maana Serikali imesikia kilio chao na kuamua kutatua tatizo la wananchi hayo.
Waziri huyo alisema kama Serikali imeweza kutoa maji kutoka Ziwa Victoria haiwezekani kushindwa kupeleka maji kwa wakazi wa Kigwa ambao wako umbali wa Kilometa 29 kutoka bomba kuu.

Profesa Mbarawa amesema mradi huo huo ukikamilika utasaidia kuwanufaisha vijiji 16 vya Jimbo la Igalula.

Alisema utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza Mwezi Desemba mwaka huu na kuongeza kuwa utekelezaji wa ujenzi wake utawahusisha vijana wa Kigwa,

Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Igalula Mussa Ntimizi aliishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kuchukua maji kutoka mradi wa bomba la Ziwa Victoria na kuwapelekea baadhi ya wakazi wa jimbo hilo ambalo lilikuwa limesaulika katika mradi wa kwanza wa kuleta maji mkoani Tabora.

Alisema hatua hiyo na ile ya kutekeleza mradi wa Tura itasaidi kuwatua ndoo wanawake wa Kigwa kama walivyoaahidi kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM yam waka 2015

Naye Mkazi wa Kigwa Dotto Mrisho alisema kuwa 2010 walijengewa tenki la maji ambapo yalitoka siku alipofika Waziri Mkuu wakati ule Mizengo Pinda lakini baada ya kuondoka hakuna maji tena toka siku ile hadi leo.

Alisema kitendo kile kiliwavunja moyo na kuona kila anapokuja kiongozi anapowaambia kuwa wataletewa maji wanajua kuwa wanadanganywa.

Mrisho alisema kuwa anaamini juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano itawasaidia kuwaondolea kero ya maji katika eneo lao la Kigwa.

Semeni Misana alisema tatizo la maji katika eneo hilo ni tatizo kubwa jambo linalowafanya waamuke usiku sana kutafuta maji ambao wakati mwingine wanakabiliwa na matatizo mengi ikiwemo kukataliwa na wenye visima.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana