Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishirika katika sala ya kumwombea marehemu kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa iliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa katika mazishi yaliyofanyika kwenye kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika sala ya kumwombea marehemu kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa iliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na baadhi ya viongozi walioshiriki katika mazishi ya marehemu kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa , Novemba 6, 2019. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Venance Mabeyo na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali, Venance Mabeyo (kushoto), Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani (kulia) baada ya wote kushiriki katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. Wa pili kulia ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
========= ========= ========
========= ========= ========
WAZIRI MKUU AFIWA NA KAKA YAKE, AWASHUKURU WALIOJITOKEZA MAZISHINI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewashukuru watu wote waliojitokeza katika mazishi ya kaka yake Mzee Bakari Majaliwa (78), aliyefariki juzi (Jumatatu, Novemba 04, 2019) nyumbani kwake katika kijiji cha Chimbila ‘B’wilayani Ruangwa, Lindi.
Ametoa shukrani hizo leo (Jumatano, Novemba 06, 2019) wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini Nandagala wilayani Ruangwa na amesema kwamba hayo ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kila mtu atapita kwenye njia hiyo.
“Tulikuwa 12 na sasa tumebaki watano, wanaume wawili na wanawake watatu. Msiba huu kwetu ni mkubwa umepunguza idadi ya watoto wa Mzee Majaliwa lakini hatuna namna ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu, wajibu wetu ni kuendelea kumuombea. Nawashukuru wote mlioacha shughuli zenu na kutukimbilia, familia imethamini sana ujio wenu jambao hili limetokea ghafla.”
Waziri Mkuu pia amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa salamu za pole alizozitoa. “Jambo hili pia limemgusa Mheshimiwa Rais wetu ambaye ametutaka tuwe watulivu katika kipindi hiki kigumu na kwamba kila mmoja kwa dhehebu lake aendelee kumuombea marehemu ili Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema.”
Amesema alipata taarifa za msiba huo wakati akijiandaa kwenda wilayani Ruangwa kwa ajili ya kushiriki mazishi yamwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa zamani wa CCM wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Kaspar Selemani Mmuya.
Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Generali, Venance Mabeyo akitoa salamu za pole kwa niaba ya Maafisa na Askari wa Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama amesema anajua uzito wa msiba pamoja na majonzi waliyonayo kwa kuondokewa na mpendwa wao na kwamba wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa ndiye anayetoa na anayetwaa. “Hakuna namna ya kurekebisha maamuzi ya Mwenyezi Mungu, tuendelee kumsindikiza kaka yetu kwa sala Mwenyezi Mungu ampokee kwa amani.”
Naye, Mwakilishi wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Othman Kaporo amesema amewataka wananchi wajiandae na kifo kwa kufanya ibada. “Ni kawaida kwa binadamu kujisahau lakini Mwenyezi Mungu ametuwekea vitu vya kutukumbusha juu ya uwepo wake ikiwemo kifo, hivyo tuyatekeleze yale yalikuwa ya wajibu kuyatekeleza.”
Post a Comment