Mike Sonko Gavana wa jiji la Nairobi ametiwa mbaroni leo huko Voi baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka wa Kenya (DPP) kuagiza kuwekwa rumande kutokana na tuhuma za uhalifu kiuchumi zinazomkabili.
Sonko anayefahamika sana kwa kuvalia vito vya dhahabu anajiunga katika safu ya maafisa wengine kadhaa wa ngazi ya juu wa serikali akiwemo Waziri wa Fedha Henry Rotich ambao hivi karibuni walihusishwa na tuhuma hizo za ufisadi na ulaji rushwa. Kamata kamata hii inatajwa kuwa ni katika juhudi za serikali ya Kenya za kupambana na ufisadi nchini.
Yassin Amaro msemaji wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi ya Kenya (EACC) amesema kuwa gavana wa Nairobi ametiwa mbaroni na maafisa wao huko Voi na kusafirishwa hadi Nairobi.

baada ya kukamatwa huko Voi
Gavana huyo wa Nairobi na maafisa wengine wa kaunti hiyo wanatuhumiwa na Noordin Haji Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka wa serikali kwamba wameinufaisha na manunuzi yasiyo ya kawaida na malipo ya kiasi cha shilingi milioni 375 za kaunti hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka wa Kenya (DPP) amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha wa kumshtaki Sonko na maafisa wengine wa kaunti ya Nairobi kwa kujipatia kinyume cha sheria mali za umma, kutakatisha fedha na jinai nyingine za kiuchumi.
Post a Comment