Featured

    Featured Posts

ANGOLA YAAHIDI KUMREJESHA DOS SANTOS

  •  Isabel dos Santos
Waendesha Mashtaka nchini Angola wamesema kuwa watatumia njia zote zinazowezekana kufanikisha zoezi la kurejeshwa nchini mfanyabiashara na binti ya rais wa zamani wa nchi hiyo, Jose Eduardo dos Santos.
Maafisa hao wamesema kuwa watatumia njia zote zinazowezekana kumrejesha nchini Isabel dos Santos, binti bilionea wa rais wa zamani wa nchi hiyo baada ya maelfu ya nyaraka zilizovuja kuonyesha madai mapya kwamba alichota mamia ya mamilioni ya fedha za serikali ya nchi hiyo.
Binti huyo wa rais wa zamani wa Angola aliyepewa jina la "mwanamke tajiri zaidi barani Afrika", anatuhumiwa kutumia nafasi ya baba yake kuiba fedha za serikali katika nchi hiyo tajiri kwa mafuta lakini iliyosalia maskini. Isabel anatuhumiwa kuiba fedha hizo za umma kwa kusaidiwa na makampuni ya ushauri ya nchi za Magharibi na kuzihamishia nje ya nchi.
Isabel dos Santos alihama Angola baada ya baba yake, Jose Eduardo dos Santos aliyetawala nchi hiyo kwa karibu miaka 40, kuondoka madarakani mwaka 2017 na nafasi yake kuchukuliwa na Joao Lourenco. Bi Isabel dos Santos aliye na umri wa miaka 46 ambaye hutumia wakati wake mwingi kati ya London na Dubai, amekanusha tuhuma hizo akisema hazina msingi wowote.
Rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos 
Akizungumza kupitia redio ya umma wiki hii, Helder Pitra Gros Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Angola amesema kuwa, watatumia njia zote zinazowezekana na kuomba msaada wa kimataifa ili kumrejesha nchini dos Santos. Amesema tayari wameomba msaada wa kimataifa kutoka Ureno, Dubai na nchi nyingine.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana