Na Saada Akida, DAR ES SALAAMMJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, Rodgers Gumbo ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamati Mashindano ya klabu huyo na Makamu wake, Rodgers Gumbo.
Taarifa ya Yanga leo imetaja wateule wa kuunda Kamati mpya ya Mashindano ya klabu hiyo baada ya wiki iliyopita uongozi kutangaza kuvunja Kamati zote zilizoundwa Novemba 25, mwaka jana.
Lakini hakuna mabadiliko hata kwenye orodha ya Wajumbe, kwani hata Katibu wa Kamati ni yule yule, Deo Mutta na Wajumbe wote wamerudi wakiwemo Wahandisi Hersi Said, Heriel Mhulo na Isaac Usaka, isipokuwa idadi imeongezeka kutoka 12 hadi 22 jumla.
Wajumbe wengine wa Kamati mpya ni Beda Tindwa, Thobias Lingangala, Edward Urio, Max Komba, Salum Mkemi, Yusuphed Mhandeni, Yanga Makaga, Adonis Bitegeko, Hassan Hussein, Pelegrinius Rutayuga, Lameck Nyambaya, Kawina Konde, Eugen Maro, Said Ntimizi, Majid Suleiman na Mussa Katabaro.
Hii inakuwa mara ya tatu uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti wake, Dk. Mshindo Msolla unavunja Kamati ya Mashindano na kuunda upya, lakini wateule wanakuwa wale wale.
Wiki iliyopita uongozi ulitangaza kuvunja Kamati zote, lakini baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo wakichapwa 3-0 na Kagera Sugar na 1-0 na Azam FC, Kamati ya Mashindano imekuwa ya kwanza ya kurudishwa.
Post a Comment