Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, litafanya kikao kesho Jumatano kutazama uwezekano wa kutangaza tahadhari ya kimataifa ya afya ya umma baada ya China kuthibitisha kwamba, kirusi hicho kinaambukizwa kupitia mawasiliano baina ya binadamu.
Tangazo hilo la WHO limetolewa baada ya mamlaka za afya nchini China kutangaza kuwa, kirusi hicho kinachofanana na kile cha SARR kimesababisha vifo vya watu 6. Meya wa eneo la Wuhan huko katikati mwa China, Zhou Xianwang amesema hadi sasa watu wasiopungua 6 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya kirusi hicho.
Jana Jumanne pia serikali ya China ilitangaza kuwa inakiweka kirusi cha sasa katika kategoria moja na kile cha Severe Acute Respiratory Syndrome (SARS) kilichoibuka mwaka 2002 na 2003 na kuua watu wasiopungua 800 katika maeno mbalimbali ya dunia.
Hatua hiyo ina maana ya ulazima wa kuwekwa karantini mtu yeyote anayepatikana na kirusi hicho na uwezekano wa kuwekekwa karantini kwa wasafiri.
Maambukizi ya kirusi hicho yaliyoanzia katika mji wa Wuhan yameeneza katika miji mingine ya China kama Beijing na Shanghai, na mamia ya watu wamepatikana na kirusi hicho.
Kesi za kirusi hichio pia tayari zimeripotiwa katika nchi nyingine kama Japan, Thailand, Korea Kusini na Australia.
Post a Comment