Featured

    Featured Posts

MAAFISA FORODHA NA WENZAO KIZIMBANI KWA UHUJUMU UCHUMI


Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MAAFISA Forodha wawili na aliyekuwa askari Polisi wa kituo cha Osterbay wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matano likiwemo shtaka la utakatishaji fedha wa sh. Milioni 57.

Mashtaka mengine wanayokabiliwa nayo ni, kuongoza genge la uhalifu, kujipatia fedha isivyo halali, kujivika uhalisia usio wao, kutumia madaraka vibaya na kutakatisha fedha.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa na wakili wa Serikali Mkunde Mshanga  akisaidiana na Gloria Mwenda imewataja washtakiwa hao kuwa ni  Edgan Foluba (Ofisa Forodha Mwandamizi), Elizabeth Mohamed (Ofisa Forodha Msaidizi), Victor Gama (dereva) askari polisi, PC Seleman Lusonzo pamoja na Mohamed Mlingo na Mrisho Kamba, 

Imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu kuwa katika tarehe isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es salaam washtakiwa wote kwa pamoja walikaa na kupanga genge la uhalifu na kusababisha kujipatia shilingi 57 milioni kwa njia isiyo halali


 Katika shtaka la pili washtakiwa hao wanadaiwa, Januari 2,2020 huko katika Manispaa ya  Ilala jijini Dar es salaam kwa pamoja walikula njama na kujipatia fedha kutoka kwa Harubu  Abdalha wakimdanganya kuwa watamsaidia kubadilisha fedha zake kwenda kwa Mkuu wa Mkoa na kuwa halali.

Aidha katika shtaka la tatu inadaiwa siku na mahali hapo,  mshtakiwa Mohamed Abdala na Mrisho Hassan katia eneo walijitambulisha kuwa ni maofisa wa serikali wanaotoka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na Mamlaka ya Mapato (TRA) huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kosa na kinyume cha sheria.

Katika shtaka la nne la matumizi mbaya ya madaraka washtakiwa, Foluba, Elizabeth na PC Lusonzo wanadaiwa Januari 2,mak.huu, wakiwa ni watumishi wa umma walijipatia kiasi cha Sh. milioni 57 kutoka kwa Haroub Abdallah wakimdanganya kuwa watampeleka kwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwa ahadi ya kumsaidia kubadilisha fedha haramu kosa walilolitenda Januari 2, 2020.

Washtakiwa wote hao poa wanadaiwa kuwa, wakiwa wamedhamiria  kujipatia Sh milioni 57 kutoka kwa Haroub Abdala walotakatisha fedha hizo wakijua wazi kuwa ni zao la fedha zilizopatikana kwa njia ya udanganyifu.

Hata hivyo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa Mahakama Kuu au mpaka DPP atakapoipa mahalama kibali cha kuweza kuisikiliza. 

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na itatajwa tena mahakamani hapo Januari 13, 2020. 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana