Featured

    Featured Posts

MAREKANI: TUPOTAYARI KUFANYA MAZUNGUMZO NA IRAN BILA MASHARTI

Kanali ya televisheni ya al-Alam imelinukuu Shirika la Habari la Reuters likiripoti kuwa,  balozi na mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ametangaza katika umoja huo kwamba, nchi yake ipo tayari kuanza mazungumzo na Iran bila masharti yoyote.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Rais wa Marekani Donald akizungumza jana katika radiamali yake kuhusiana na mashambulio ya makombora ya Iran dhidi ya kambi za kijeshi za nchi hiyo nchini Iraq alidai kuwa, hakuna raia wa Iraq au Marekani aliyeuawa katika shambulio hilo japo kambi hizo ziliharibiwa kidogo. Trump alidai kwamba, "Iran inaonekana kurudi nyuma, hatua ambayo ni nzuri kwa pande zote husika.
Hata hivyo alisema kuwa, ataongeza vikwazo dhidi ya Iran. Hatua ya kuchelewa ya Trump ya kuzungumzia mashambulio ya makombora ya Iran dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani huko Iraq na kujaribu kuonyesha kwamba, mashambulio hayo hayakusababisha hasara kubwa, imetajwa na wajuzi wa mambo kuwa ni kulegeza msimamo Marekani hasa ikizingatiwa kuwa, ilikuwa ikitoa matamshi makali kwamba, itachukua hatua kali endapo Iran ingelipiza kisasi cha kuuawa Luteni Jenerali Qassim Soleimani.
Wakati Rais Trump akidai kwamba, hakuna mwanajeshi wa Marekani aliyejeruhiwa au kuuawa katika shambulio hilo afisa mmoja mwandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, zaidi ya magaidi 80 wa jeshi la Marekani wameang amizwa na karibu 200 wengine wamejeruhiwa katika majibu makali yaliyotolewa na Iran dhidi ya kambi mbili za kijeshi za nchi hiyo huko Iraq.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana