Mama yake Rajab Abdulkahari a.k.a Harmonize aitwaye Habiba Chivalavala akikabidhi mashuka kwa DC wa Tandahimba Sebastian Waryuba kwa ajili ya hospital ya Wilaya
Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba (katikati)akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Omary Nang'uta na Mama Harmonize
Wananchi ambao walijitokeza katika makabidhiano hayo wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Tandahimba Hawa Ramadhani(CCM viti maalum)
Mashine ya kusaidia kupumua kwa wagonjwa ambayo imetolewa na Msanii Harmonize.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amepokea mashine ya kupumulia na mashuka vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 10 kutoka kwa Msanii Rajabu Abdulkahari (Harmonize)
Vifaa hivyo ambavyo vimekabidhiwa na mama yake Habiba Chivalavala amesema vitasaidia wagonjwa katika hospitali ya Wilaya
"Tunashukuru kwa vifaa hivi ambavyo ni muhimu kwa wagonjwa mashuka 48 na mashine ya kupumulia,nami nawakabidhi idara ya Afya ili vikatumike,amesema Waryuba,"
Naye mama Harmonize amesema kuwa anafarijika kwa mwanaye kurudishia kile anachokipata kwa wananchi hususan huku ambako amezaliwa
"Nafarijika nikiona anatambua umuhimu wa kuwakumbuka wengine hususan hospital sehemu ambayo haikwepeki,"amesema mama Harmon
Post a Comment