Featured

    Featured Posts

NEWS ALERT: MAHAKAMA YAPIGILIA MSUMARI UMEYA JIJI LA DAR, YATUPILIA MBALI MAOMBI YA ISAYA MWITA


Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita.
 
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
AMEGONGA mwamba!Ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali maombi ya Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ya kutetea nafasi yake ya Umeya wa Jiji hilo.

Mahakama imesema leo kuwa haiwezi kutoa amri ya kumzuia Meya huyo asiondolewe madarakani kwa sababu katika maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo hayana uthibitisho kuhusu uwepo wa kikao cha wajibu maombi ambao ni Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam cha kumwondoa madarakani wala hasara atakayopata kama amri hiyo haitotolewa.

Hoja za Wakili wa muombaji hazina miguu ya kusimamia kwa kushindwa kufata vigezo ikiwemo uwepo wa kikao cha kutaka kumtoa madarakani," amesema Hakimu Mtega.

Uamuzi huo umetolewa leo Januari 10,2020 ikiwa ni siku moja baada ya Mwita kuvuliwa madaraka hayo kupitia kikao cha Baraza la Halmashuri, huku Mwita akidai akidi haijatimia na yeye bado Kiongozi.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana