RAIS DK. MAGUFULI AWASILI KUSHIRIKI SHEREHE ZA MIAKA 56 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Rais Dk. John Magufuli amewasili leo mjini Zanzibar kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tano kisiwani hapa, ambapo pia atashiriki Sherehe za Maadhimisho ya miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, zitakazofikia kilele chake keshokutwa, Jumapili Januari 12, 2020. Pichani, Rais Dk. Magufuli, akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi, alipowasili na kulakiwa na viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume mjini Unguja, leo. >>> PICHA ZA IDI BOFYA HAPA
Post a Comment