Seneta wa jimbo la Virginia nchini Marekani amesema kuwa, katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2016, Rais Barack Obama wa wakati huo alimtaja Donald Trump kuwa ni Mfashisti.
Tim Kaine aliyasema hayo Jumapili ya jana na kuongeza kuwa katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2016, na katika mazungumzo yake aliyoyafanya na rais huyo wa zamani wa Marekani, alimtaja Trump kuwa ni Mfashisti. Kaine ameongeza kuwa katika kipindi hicho cha kampeni Obama alimpigia simu na kumueleza kwamba: "Tim Kaine kumbuka kuwa hivi sasa sio wakati wa kutokuwa na busara, ni lazima kumuondoa Mfashisti White House." Kinyume na alivyo Trump, Obama wakati alipoondoka ikulu na kumkabidhi madaraka Donald Trump ni mara chache sana amemzungumzia vibaya rais huyo wa sasa.
Hivi karibuni Barack Obama alinukuliwa akisema kuwa hivi sasa kumeongezeka tabia ya upotoshaji wa jamii nchini Marekani kati ya wanasiasa na kwamba suala hilo linatishia nchi hiyo. Baadhi wanaamini kwamba maelezo ya rais huyo wa zamani wa Marekani yalikuwa yanamlenga Rais Donald Trump.
Post a Comment