Featured

    Featured Posts

RAIS DK. MAGUFULI AMTWISHA ZIGO SIMBACHAWENE, AMUAGIZA KUNG'OA VIONGOZI NA WATENDAJI AMBAO NI KIKWAZO WIZARA YA MAMBO YA NDANI

Rais Dk. John Magufuli akimuapisha George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Ikulu

IKULU, DAR ES SALAAM
Rais Dk. John Magufuli amewaapisha George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mussa Azzan Zungu kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Pia amewapisha Maimuna Kibenga Tarishi kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva – Uswisi, Hussein Athuman Kattanga kuwa Balozi wa Tanzania Tokyo, Japan na Prof. Kennedy Godfrey Gastorn kuwa Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa New York, Marekani.

Akizungumza baada ya kuwaapisha na kushuhudia wakila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma, Rais Magufuli amewataka viongozi hao kwenda kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uchapakazi, kutanguliza maslahi ya Tanzania pamoja na kushirikiana vizuri na viongozi na watendaji wengine katika wizara zao.

Amemtaka Waziri Simbachawene kushughulikia dosari zilizopo katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwemo kuhakikisha watendaji na viongozi ambao ni kikwazo katika ufanisi wa wizara wanaondolewa, pamoja na kushughulikia makubaliano yaliyotiwa saini na viongozi wakuu wa wizara waliopita kuhusu mkataba wa ununuzi wa vifaa vya zimamoto (vyenye thamani ya zaidi ya sh. Trilioni 1) katika mazingira yasiyokuwa na uadilifu na bila kujali maslahi ya Taifa.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam na imehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana