Mpango huo umetangazwa na rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky ambaye amesema pia atalazimisha Iran kutoa kiwango kingine cha fedha kitakacholipwa kama fidia kwa familia za wahanga.
Watu 176 wakiwemo raia 11 wa Ukraine walikufa wakati ndege ya shrika la Ukriane chapa Boeing 737 ilipoanguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege mjini Tehran.
Hapo jana maafisa wa Iran walikiri ndege hiyo ilianguka baada ya kushambuliwa kwa bahati mbaya na kombora la jeshi la Iran.
Rais Zelensky alizungumza kwa njia ya simu na rais Hassan Rouhani wa Iran ambaye ameahidi nchi yake itawafungulia mashtaka wote waliosababisha kutokea ajali hiyo.
Post a Comment