Karibu watu 35 wameripotiwa kufarika kufuatia kisa cha mkanyagano katika mazishi ya Qasem Soleimani, jenerali wa kikosi maalum cha jeshi la Iran alieuawa na Marekani wiki iliyopita.
Zaidi ya watu 40 pia wamejeruhiwa katika kisa hicho kilichotokea mjini Kerman, kwa mujibu wa ripoti hizo.
Qasem Soleimani anazikwa leo nyumbani kwake ambako mamilioni ya watu wamekusanyika barabarani kumuaga.
Mauaji yake yameibua hofu ya kuzuka kwa mzozo kati ya Marekani na Iran.
Post a Comment