Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha vifungu 55 vya muongozo utakaomaliza vita nchini Libya na kushutumu ongezeko la matumizi ya nguvu katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta ya Afrika ya kaskazini.
Azimio lililoidhinishwa na baraza la Usalama pia limetoa wito wa kuwapo na usitishaji wa kudumu wa mapigano nchini Libya, ambako makubaliano tete ya kusitisha mapigano yamekuwapo tangu Januari mwaka huu.
Azimio hilo lililotayarishwa na Uingereza , liliidhinishwa kwa kura 14 kati ya 15, ambapo Urusi imejizuwia kupiga kura, licha ya kuwa rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwa mmoja wa viongozi 12 waliokubaliana na mpango huo katika mkutano mjini Berlin Januari 19.
Balozi wa Urusi katika Umoja wa mataifa Vassily Nebenzia amesema amejizuwia kupiga kura kwasababu serikali yake ina wasiwasi mkubwa , juu ya iwapo azimio hilo linaweza kutekelezwa na kumaliza vita kati ya serikali hasimu, katika njia ambayo tungependa kuiona.
"Tuna wasi wasi mkubwa iwapo aina hii ya kauli ya mwisho itawawezesha Walibya kufikia makubaliano haraka. Kwa kweli tungependa maazimio ya baraza la Usalama kutekelezwa. Tungependa azimio hili lifanyekazi. Hata hivyo sidhani kama maelezo ya azimio hili yanawezekana.
Wapiganaji wa majeshi ya serikali inayoungwa mkono kimataifa mjini Tripoli wakijitayarisha kwa mapambano
"Matukio yataonesha nani yuko sahihi," amesema Nebenzia. Na iwapo azimio hilo litakuwa na athari chanya katika kutatua mzozo huo, nitakuwa wa kwanza kukiri kwamba nilikosea."
Azimio hilo limesisitiza , "haja ya kuwapo na usitishaji wa kudumu ya vita nchini Libya haraka iwezekanavyo, bila ya masharti yoyote. Pia azimio hilo limeeleza wasi wasi kuhusu ongezeko la kuhusika kwa wapiganaji mamluki nchini Libya.
Naibu mwakilishi wa kudumu wa Ujerumani katika Umoja wa Mataifa Juergen Schultz amesema azimio hilo linatuma ujumbe kwa Libya.
"Kwa kuidhinishwa azimio hili, baraza la Usalama linatuma ishara muhimu kwa amani nchini Libya, likisisitiza nia sahihi ya washiriki wote wa mkutano wa Berlin. Ni muhimu kwa Libya kwamba tumeweza kutuma ishara hii ya Umoja."
Balozi wa Uingereza amepinga kauli ya balozi wa Urusi na kusema azimio hilo linawezekana, akisema kile inachokifanya , ni kutoa maelezo sahihi ya nia ambazo viongozi waliidhinisha mjini Berlin, na hii ni pamoja na rais Putin wa Urusi.
Post a Comment