Taarifa iliyotolewa mapema leo na Wizara ya Ulinzi ya Russia imeashiria utumaji silaha kwa magaidi walioko katika eneo la Idlib, unaofanywa kutokea Uturuki na kueleza kuwa, hali ya wasiwasi inayoshuhudiwa Idlib imejitokeza baada ya magaidi kushambulia maeneo yaliyoko jirani na mkoa huo wa kaskazini magharibi mwa Syria.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa, magaidi walioko Idlib wanapewa misaada na msukumo kutoka nje; na silaha na zana za kivita zimekuwa zikiingizwa katika eneo la amani la Idlib kupitia mpaka wa pamoja wa Uturuki na Syria.
Hali ya usalama katika eneo la amani la Idlib imevurugika katika wiki za karibuni kutokana na harakati za magaidi na mashambulio wanayofanya kulenga eneo hilo na sehemu zingine za ardhi ya Syria.
Baada ya Uturuki kuingiza wanajeshi wake pamoja na zana za kivita kinyume cha sheria ndani ya ardhi ya Syria, sambamba na magaidi inawaounga mkono kukiuka mara kwa mara usitishaji vita uliofikiwa katika eneo hilo, hivi karibuni jeshi la Syria liliamua kutekeleza operesheni za kijeshi na kukomboa zaidi ya nusu ya maeneo yaliyokuwa mikononi mwa magaidi hao.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, jeshi la Uturuki pia limevamia na kushambulia mara kadhaa ardhi ya Syria, ambapo mara zote hujuma na uvamizi huo umelaaniwa vikali kimataifa na kukabiliwa na jibu na radiamali ya wananchi na serikali ya Syria.../
Post a Comment