Featured

    Featured Posts

CHADEMA YAZIDI KUMEGUKA VIPANDE


  Aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi/ Uhamasishaji  wa Baraza la Vijana la Chama Cha demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), Edward Simbeye Leo  February 26, 2020 ametangaza kujivua uanachama wa CHADEMA, kwa kile alichokisema kutokuunga mkono baadhi ya mambo yanayoendelea ndani ya chama hicho cha Chadema na kwamba kwa sasa anatafakari chama gani cha kujiunga.

Sembeye amesema moja ya vitu vinavyokiumiza chama hicho, ni chama  kuendeshwa kwa amri na matakwa ya  Freeman Mbowe ambaye ni  mwenyekiti wa chama hicho na si Katiba ya Chadema. 

“Kila chama cha siasa duniani kina malengo yake na moja ya malengo ni kuchukua dola, lakini Chadema imetoka kwenye malengo ya msingi ya kuchukua dola badala yake kimekuwa kikundi cha watu wachache na badala ya kuwa chama cha siasa imekuwa kampuni ya mtu binafsi

"Mambo ya Chadema yanatakiwa kuamuliwa kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na miongozo ya chama, leo yanaamuliwa kwa kauli na amri za Mbowe, Mwenyekiti ameamua kugeuza chama kuwa mali yake binafsi, lakini tukitoka nje tunawaaminisha umma kuwa chama hichi ni mali ya Watanzania.

“Siioni ‘future’ ya Chadema kuwa chama mbadala wa CCM, mwaka 2014 Chadema ilishinda zaidi ya vijiji na vitongoji na mitaa 1, 000 lakini tunavyozungumza sasa Chadema haina kijiji hata kimoja na tunakwenda kwenye Uchaguzi Mkuu na haina kijiji hata kimoja

“Mwaka 2015 tumepata wabunge katika majimbo si chini ya 35 ila hadi sasa zaidi ya asilimia 32 ya wabunge wa Chadema wameondoka kwenye chama, hatuna wabunge 11 na sio hao tu kuna wengine wengi zaidi wataondoka muda utakapofika  

“Kuna mambo yanazungumzwa kwamba baadhi ya watu wanaoondoka wananunuliwa lakini jambo la kujiuliza hivi kweli utu wa mtu unaweza kununuliwa? ni lini kama Chama wamewahi kutafuta sababu ya msingi ya watu kuondoka na kila kukicha watu wanaondoka na hawasemi ukweli.

“Mwaka 2015 Lowasa alipofika kwetu akagombea urais alitusaidia kupata asilimia 40 ya kura, tuliaminiwa hadi Kimataifa kuwa Chadema inaweza kupewa nchi, leo hii Lowasa ameondoka mnasema ameondoka na mkewe tu mkumbuke alikuwa Waziri Mkuu na hiyo ni taasis.

“Tukija kwa Sumaye tulimdaharirisha sana hakuna asiyejua namna ambavyo tumemdharirisha, alipofika kwetu alitusaidia kufungua milango kwa nafasi yake aliyonayo, leo tunambeza, tunamkejeli na kumuona hana maana katika chama na had tunaimba mapambio kuwa tuko imara.

“Leo tunazungumza tumeondokewa na Katibu Mkuu Mashinji ambaye alikuwa rafiki yangu sana, ameondoka kwenda CCM na hatuelezwi sababu za kina za kuondoka kwake, leo tunasema alikuwa msaliti hakuna aliyekuwa anamjua Mashinji na aliyemleta ni Mbowe sasa anakuwaje msaliti-Amesema
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana