Featured

    Featured Posts

MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI WAPITISHA BAJETI YA TSH. BILIONI 37.3

Na Hamisi Abdulrahmani, Masasi.

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, limepitisha mapendekezo ya makisio ya mapato na matumizi ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/ 2021 ya Sh.bilioni 37.3

Bajeti hiyo, imekuwa na ongezeko la asilimia 44.5 ukilinganisha na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2019/2020 ambapo bajeti hiyo, ilikuwa ya Sh.bilioni 25.

Akisoma bajeti hiyo jana wakati wa kikao cha baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo lililoketi kwa ajili ya  kujadili na kupitisha makisio hayo ya bajeti, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Masasi, Juma Satma amesema ili kufanikisha utekelezaji wa bajeti hiyo ni lazima watendaji waongeze juhudi na uadilifu katika ukusanyaji wa mapato.

Alisema  iwapo bajeti hiyo ikifanikiwa kwa asilimia 100 itasaidia kuweza kutekeleza shughuli mbalimbali za kimaendeleo zilizopangwa na halmashauri hiyo.

Satma alisema bajeti hiyo itafanikiwa iwapo vyanzo vyake mapato ya ndani vitasimamiwa kikamilifu katika ukusanyaji wa mapato.

Alisema bajeti hiyo ya mwaka 2020/2021 ya sh.bilioni 37.3 imekuwa na ongezeko la asilimia 44.5 ukilinganisha na makisio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020 ya sh.bilioni 25

Alisema katika bajeti hiyo ya mwaka wa fedha 2020/2021 yapo mapato yatakatotokana na mapato ya ndani, fedha kutoka serikali kuu na michango ya wahisani mbalimbali.

"Tuna vyanzo vingi vya mapato katika halmashauri yetu lakini fedha hatuzioni huku ukifutilia tunaona zinakusanywa ipo haja ya kuwafutilia hawa watendaji tujuwe nani anajinufaisha fedha za mapato," alisema Satma

Arafati Kokocha diwani wa kata ya Mbuyuni( CCM) alisema licha ya halmashauri hiyo kupanga bajeti hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo lakini wapo baadhi ya watendaji wamekuwa wakikwamisha.

Alisema bado kumekuwa na mianya mingi ya upotevu wa mapato ya halmashauri katika vyanzo vyake vya mapato kutokana na watendaji kuonekana kuwa wanajinufaisha mapato ya halmashauri.

Naye Mashaka Salumu diwani kata ya Namajani(CCM), alisema bado kuna udhaifu mkubwa katika kitengo cha mapato hasa katika eneo la ukusanyaji mapato.

Alisema halmashauri kila siku imekuwa na kilio cha mapato lakini ukiangali vyanzo vipo vya ukusanyaji mapato na fedha zinakusanywa ila hazijulikani zinakokwenda.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Masasi iwapo watendaji wataendelea kuwa na hali ya ufanyaji kazi kwa kujituma hata maendeleo yanapatikana kwa haraka.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana