Featured

    Featured Posts

MAHAKAMA KUHARAKISHA USIKILIZAJI WA MASHAURI-ARUSHA


 SP Mikidadi Galilima - Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Arusha akimuongoza mgeni rasmi kukagua gwaride   Mhe.Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Arusha Moses Gunga Mzuna akiongozana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana

 Gwaride maalum lililoandaliwa na Jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Kwaajili ya maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini katika viwanja vya Mahakama ya mwanzo Arusha Mjini




 Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama kuu Arusha Sekela Mwaiseje akizungumza katika siku ya Maaadhimisho ya siku ya sheria Mahakama ya Mwanzo Arusha Mjini
SP Mikidadi Galilima - Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Arusha akitoa salamu kwa  Mhe.Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Arusha Moses Gunga Mzuna kushoto kwake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana
Mhe.Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Arusha Moses Gunga Mzuna kushoto kwake ji mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakiwa katika Maadhimisho ya siku ya sheria nchini katika Mahakama ya Mwanzo Arusha Mjini.
Kutoka kushoto ni Mhe.Pamela Meena Hakimu Mahakama ya hakimu mkazi akiwa na wenzake katika kilele cha maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Arusha Mjini
Baadhi ya Mhakimu wakiwa katika siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika Mahakama ya mwanzo Arusha Mjini leo

Na Vero Ignatus, Arusha

Maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini yamefanyika leo katika viwanja vya Mahakama ya mwanzo Mjini Arusha ambapo madhumuni yake ni kuashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Mahakama,sambamba na kuelimisha jamii kwa kuzingatia mada na iliyotolewa kwa mwaka husika

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha Moses Gunga Mzuna  alisema kuwa kazi kuu ya na wajibu wa msingi wa Mahakama ni kutoaji haki kwa watu wote ambapo suala hilo siyo mambo ya Kisheria peke yake bali ni suala la Kikatiba.

Mhe.Mzuna alisema Mahakama inatazamiwa kuharakisha usikilizaji wa migogoro inayohusiana na wawekezaji na ya kibiashara ili hatima yake ifahamike mapema iwezekananyo na hivyo kuruhusu shughuli nyingine za kimaendeleo na ukuaji wa uchumi kuendana sawa na dira ya serikali.

“Hivyo basi serikali imejitahidi kurekebisha mfumo wa uchumi kulingana na mazingira ya uchumi wa soko na utandawazi ikiwemo kuweka mazingira ya kuwavutia wawekezaji mbalimbali vilevile mahakama inatakiwa iende sambamba na mabadiliko hayo ambayo yanagusa eneo muhimu la utoaji haki

Aidha alisisitiza kuwa Mahakama imeweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa mashauri hayachukui muda mrefu wala kuahairishwa pasipokuwa na sababu za msingi ambapo katika Mahakama za mwanzo mashauri hayapaswi kukaa zaidi ya miezi sita, wakati katika  Mahakama za Hakimu Mkazi wa wilaya mashauri hupaswa kuchukua muda wa miezi kumi na mbili kukamilika na kwa upande wa Mahakama Kuu shauri halitakiwi kukaa si zaidi ya miaka miwili.

''Kuthibitisha hili kwa mahakama Kuu Arusha mwaka juzi (2018)Mashauri yaliyomalizika yalitumia wastani wa siku 347 kwa mwaka 2019 ni wastani wa siku 397kwa muda wa miaka hiyo miwili wastani wake ni siku 374 sawa na mwaka mmoja na mwezi mmoja (1.022185)’’Alisema

  Nae Mkuu wa Mashtaka mkoa wa Arusha Abdallah Chavula  mfumo huru na madhubuti wa haki jinai katika ukuaji wa uchumi ni kuongeza usalama wawananchi na kupunguza uhalifu sambamba na kupunguza gharama za kiuchumi kwa serikali kutotumia uhalifu na kupunguza gharama kwa serikali kutotumia fedha na rasilimali katika kulinda jamii na mali zao dhidi ya vitendo vya kihalifu

Chavula alisema kuwa matunda ya mfumo huo ni uwepo wa amani na utulivu katika jamii hivyo shughuli za uwekezaji na biashara kuweza kufanyika kwa wepesi na mchango wawaendesha mashtaka katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara ili kusimamia na kuratibu kwa weledi shughuli za upelelezi,kuakikisha mashtaka yanayofunguliwa mahakamani ni yale ya yenye ushahidi madhubuti na kuendesha mashauri ya jinai bila ubaguzi wala upendeleo  

Nae Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama kuu Arusha Sekela Mwaiseje alisema kuwa katika wiki ya Sheria Mahakama na wadau wametoa elimu ya sheria sehemu mbalimbali ikiwemo Mrisho Gambo sekondari,Muungano ,Ilboru,Chuo cha kilimo na mifugo Tengeru Chuo cha Ufundi Arusha pia elimu hiyo imetolewa katika vyombo mbalimbali vya habari mkoani hapa

Elimu hiyo iliyotolewa na mahakama imewafikia wastani wa wananchi 2565 ambapo hesabu hiyo haijajumuisha wananchi mbalimbali ambao walisikiliza kupittia vyombo vya habari
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana