Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye ametangaza kujiuzulu kuanzia Machi 31, 2020 baada ya kuitumikia taasisi hiyo kwa miaka nane.
Jana Ijumaa Februari 7, 2020 kwa niaba ya bodi ya wakurugenzi, kaimu mwenyekiti wa taasisi hiyo Angelina Ngalula alitoa taarifa ya kujiuzulu kwa Simbeye.
“Kwa niaba ya bodi ya wakurugenzi napenda kuwataarifu wanachama wa TPSF, wabia, wadau na umma kwa ujumla juu ya kujiuzulu kwa Simbeye..., Simbeye alikuwa na mchango mkubwa sana kwa taasisi yetu tangu alipojiunga nayo,” anaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Ngalula amesema Simbeye aliyehudumu nafasi hiyo tangu mwaka 2012 amejiuzulu ili apate muda wa kutekeleza majukumu yake mengine.
Taasisi hiyo imemshukuru kwa utumishi wake na kumtakia kila la kheri katika mambo anayokusudia kuyafanya.
Post a Comment