Featured

    Featured Posts

MUFTI WA TANZANIA AWATAKA WAISLAMU KUWA WATULIVU KWA KUCHANWA QUR-ANN

  Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewataka Waislamu nchini kuwa watulivu wakati vyombo vya sheria vikiendelea kuchukuwa hatua kwa tukio la kuchanwa kwa Quran.

Amesema kuwa kitendo cha kuchanwa kwa kitabu kitukufu cha Quran kilichofanywa na Afisa Biashara wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Daniel Malaki hakihusiani na mitazamo yoyote ya kidini bali ni utashi wake binafsi

Ameongeza kuwa kitendo hicho ni cha uzalilishaji wa maneno ya Mungu yanayopelekea kuwaudhi Waislamu na kusababisha kuleta mfarakano miongoni mwa jamii.

“Niwaombe Waislamu kuendelea kuwa na subira na uvumilivu huku wakisubiri kauli za viongozi wao wa Bakwata ambao wanafuatilia kwa ukaribu kesi iliyopo mahakama kwa sasa, “amesema Mufti Zubeir.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana