Featured

    Featured Posts

PENTAGON YATAHADHARISHA ONGEZEKO LA KUJIUA ASKARI KIKOSI CHA ANGA MAREKANI

Katika indhari mpya ya Pentagon kuhusiana na ongezeko la kujiua askari wa nchi hiyo, viongozi wa jeshi la anga wametangaza kuwa kiwango cha kujiua ndani ya jeshi hilo kiliongezeka kwa asilimia 33 mwaka 2019 ikilinganishwa na mwaka 2018. Jeshi la anga la Marekani pia limeongeza kuwa jumla ya askari 137 wanaohudumu katika jeshi la anga na ambao ni walinzi wa taifa na akiba ya jeshi la anga walijiua mwaka jana. Brian Kelly, kaimu mkuu wa kitengo cha nguvu kazi, wafanyakazi na huduma za jeshi la anga nchini Marekani amesema kuwa, sio rahisi kufahamu njia za kukabiliana na ongezeko la kujiua kwa askari hao.
Ongezeko la kujiua kati ya askari wa Marekani
Hadi sasa Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetoa ripoti mbalimbali kuhusiana na ongezeko la vitendo vya kujiua askari wa nchi hiyo hasa katika miaka ya hivi karibuni. Viongozi wa kijeshi nchini humo wanayataja matatizo ya kisaikolojia kwa askari waliorejea kutoa maeneo ya vita kuwa chanzo kikuu cha kujiua askari hao.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana