Featured

    Featured Posts

UBOVU WA BARABARA WAKATISHA ZIARA YA NAIBU WAZIRI

Na James Timber, Mwanza.

Ubovu wa barabara uliopo Kata ya Bugogwa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, umesababisha msafara wa Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi, Eliasi Kwandikwa kutoendelea na ziara kama ilivyopangwa.

Hali hiyo iliyozua sintofahamu katika ziara hiyo ilitokana na baadhi ya magari yaliyo kwenye msafara huo kukwama kwenye tope na mabonde na hivyo kuifanya ziara hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mwenyeji ambaye ni Mbunge wa jimbola Ilemela, Angeline Mabula kushindwa kufika katika eneo lengwa ambapo imejengwa hospitali ya wilaya ya ilemela.

Akizungumuzia taharuki hiyo ya ubovu wa barabara hizo Naibu Waziri Kwandikwa alisema kilichotokea na sehemu ya kazi iliyowaleta kwani ziara yake ililenga kujionea kwa macho hali halisi ya miundombinu katika halimashauri hiyo ambayo inakua kwa kasi kutokana na ongezeko la shughuli za kiuchumi pamoja na mahitaji ya huduma za kijamii.

Kwandikwa amesema ofisi yake kwa kushirikiana na halmashauri zote nchini Ilemela ikiwa mojawapo inaendelea kusimamia uboreshwaji wa miundombinu yote hasa barabara ili kuweka  mazingira rafiki kwa huduma zingine za kijamii kufikiwa kwa urahisi na wananchi wa maeneo husika.

"Kama mlivyoona leo hii katika ziara yangu nililenga kufika katika hospitali ya wilaya ya Ilemela iliyijengwa ili kuona jinsi gani tunaweza kujenga miundombinu ambayo itawarahisishia wananchi kuifikia hospitali hiyo lakini kwa bahati mbaya tumeshindwa kulifikia eneo husika kutokana na ubovu wa barabara.

"Hii yote ni ishara tosha kuwa tunayo haja ya kuboresha barabara hizi ili huduma zitakazokuwa zinapatikana kwenye hospitali hiyo na maeneo ya karibu zifikiwe kwa urahisi na kwa kuwa nimejionea kwa macho na kwa matendo nadhani ofisi yangu italifanyia kazi ili kuondoa kero  ya ubovu huu wa barabara katika halmashauri hii ya ilemela.

"Lakini niwakumbushe tu kwamba Halmashauri ya Ilemela inaziwakilisha Halmshauri nyingi nchini zinazokumbwa na ubovu wa barabara hasa katika kipindi hiki cha mvua ila niwakikishie wabunge na wakuu wa wilaya wote nchini kuwa serikali yetu inaendelea kufanya kile liwezekanalo kuondoa kero hii ya ubovu wa barabara na tutafika kila eneo kutatua changamoto hii," amesema  Kwandikwa.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Ilemela, Angelina Mabula alimushukuru Naibu waziri kwa kutembelea eneo lake na kujione kwa macho changamoto zilizopo katika sekta ya miundombinu hasa barabara hivyo ana imani italowa ufumbuzi baada ya ziara hiyo.
Aidha Mabula alisema Ubovu wa barabara uliokwamisha ziara ya Naibu waziri umetokana na barabara hiyo kuwa bado haijajengwa na bado inafanyiwa tasmini ili kufikia adhimio yatayomuleta mkandarasi katika eneo hilo ili kuanza kazi kwani barabara hiyo ni muhimu sana katika halmashauri yake kutokana na kuwa ndio njia inayoelekea katika hospitaliya halmashauri ambayo imeshajengwa.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana