Featured

    Featured Posts

UFUGAJI MBWA WAMPA KIJANA UTAJIRI MKOANI KAGERA

Na Lydia Lugakila Kagera:-

Kijana mkoani Kagera aliyepambana na ukosefu wa ajira  kwa muda mrefu afanikiwa kujiajiri na kutoa ajira kwa vijana 1000 asimulia ufugaji wa mbwa na kilimo cha miti kumpatia utajiri atoa neno kwa serikali.

Kijana huyo Evance Kamenge amebainisha hayo mbele ya Naibu waziri ofisi waziri mkuu Kazi, Vijana, Ajira Sera na watu wenye ulemavu Anthony Mavunde katika kongamano la umoja wa vijana CCM mkoani Kagera lililofanyika katika ukumbi wa Linas uliopo manispaa ya Bukoba na  kuwakusanya vijana toka wilaya nane za mkoa huo.

 Kamenge amesimulia  alivyopambana na suala la ajira pamoja na kipato hadi kufikia hatua ya kujipatia ajira yeye mwenyewe kisha kuajiri vijana 1000.

Kijana huyo ambaye kwa sasa ni  mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya kilimo amesema ameamini ajira sio ofisini.

Hatua hiyo imekuja kufuatia vijana wengi kulilia ajira kila kukicha na kubaki kuilaumu serikali.

Kijana huyo amesema mwanzoni alianza na ufugaji wa Samaki na kuku akiwa anasambaza bidhaa hiyo jijini Dar es salaam ambapo baadae akajikita katika ufugaji wa Ng'ombe ambapo pia aliaweza kusambaza  maziwa jijini Dar es salaam na kupata mafanikio makubwa na kuamua kuanzisha biashara ya ufugaji wa mbwa wa aina mbali mbali kutoka Afrika kusini na sasa ni msambazaji wa wanyama hao ndani na nje ya Nchi kama Zimbabwe, Zambia.
Amesema biashara hiyo ya mbwa imependwa sana na watu kutokana na kuwatumia  kwa ajili ya ulinzi wao binafsi na katika makampuni mbali mbali.

Amesema hadi sasa taswira ya maisha yake imebadilika sana ambapo akiwa mkoani Kagera katika harakati za kilimo cha miti maharage na mahindi ametoa ajira 1000 kwa vijana.

Akitaja kuboresha ufugaji wa mbwa amesema tayari kwa mkoa wa Kagera ameanzisha ofisi yake maeneo ya Custom ambapo ameanza kujenga mabanda ili kushawishi vijana kuingia katika ufugaji wa mbwa.

"Mbwa ni uchumi mbwa ni fulsa nimepata gari, nimejenga nipo katika harakati za kuendesha shule moja hapa Kagera na nitatoa mafunzo kwa vijana juu ya kuendesha miradi mbali mbali "lisema Kamenge.

Aidha amemuomba waziri  Mavunde kuhakikisha Wizara hiyo inatambua mashindano kama ya kwake yaliyoleta mafanikio kwa vijana 1000 kupata ajira.

Kijana huyo amekiri kuwa kilimo ni utajiri sasa kilimo na ufugaji wa mbwa vimefanya  maisha ya Kijana Evance Kamenge kuwa tajiri.

Kwa upande wake Naibu waziri huyo amepongeza juhudi za kijana huyo na kuahidi kuzungumza naye kwani tayari amekuwa mdau mkubwa kutokana na upambanaji huo.

Waziri Mavunde amesema bado ipo changamoto kubwa kuwakusanya vijana watano mpaka kumi wenye mlengo mmoja na kuwa baadhi ya maeneo vikundi vingi hushindwa kuendelea ambapo uchukua mkopo na kwenda kugawana na kisha kununua nguo na viatu badala ya kuwekeza katika shughuli za maendeleo.

Hata hivyo waziri huyo amesema serikali itaendelea kuwasaidia vijana wote wakiwemo wenye ulemavu kwa kufanya marejeo ya kanuni za utoaji mikopo ikiwemo kuwakusanya vijana katika makundi ili wanufaike na fursa mbali mbali.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana