Idadi ya vifo kutokana na janga la virusi vya corona nchini China imefikia watu 304 kufikia jana usiku, baada ya watu 45 kufariki dunia katika siku iliyotangulia.
Tume ya Afya nchini humo imesema vifo hivi vipya vilitokea katika mkoa wa Hubei, ambao ndio kitovu cha mlipuko wa virusi hivyo.
Kote nchini China, kulikuwa na maambukizi mapya ya watu 2,590 jana Jumamosi na kufikisha 14,380 jumla ya idadi ya watu walioambukizwa mpaka sasa.
China inaendelea kutengwa wakati hatua za kudhibiti usafiri duniani zikiendelea kuchukuliwa na kufutwa safari za ndege.
Janga hilo limesababisha mataifa mengi kuwahamisha raia wao huku mashirika ya ndege yakisitisha safari kwenda nchini humo.
Hatua hiyo pia inatishia kuathiri kwa kiasi kikubwa kushuka uchumi wa taifa hilo la pili kwa ukubwa kiuchumi duniani.
Kumeripotiwa zaidi ya visa 130 vya maambukizi ya virusi vya corona katika karibu nchi nyingine 24 duniani.
Post a Comment