Watu sita, wawili wakiwa ni mama na watoto wao wamefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kuchomwa moto usiku wa manane na kuteketea katika kitongoji cha Uponda kata ya Mjawa wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Akizungumza kwa njia ya simu kwa niaba ya kamanda wa mkoa wa kipolisi Rufiji kamishna mwandamizi Onesmo Lyanga mwakilishi wake kamishna msaidizi Richard Ngolle amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na mtuhumiwa Richard Mathias mkazi wa Buza Dar es Salaam na Masasi mkoani Mtwara anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Rufiji kwa tuhuma hizo.
Akielezea tukio lilivyotokea bila kuingia kwa undani amesema ni wivu wa mapenzi kati ya Bi.Regina avondo ambaye kwa sasa ni marehemu na mpenzi wake Bw.Richard Mathias aliyekwenda nyumbani kwa mpenzi wake marehemu Regina Mavondo usiku wa manane tarehe 8/2/2028 na kuchoma nyumba yake ambayo ndani kulikuwa na watu wengine watano wamelala wawili wakiwa ni watoto wa mdogo wake marehemu Regina Mavondo.
Post a Comment