<<Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye akiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally baada kuingia nae ukumbini kwenye Kikao Maalum cha Baraza la Wadhamni wa Chama Cha Mapinduzi, kinachofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Lumumba, Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye leo ametinga Ofisdi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lumumba jijini Dar es Salaam, na kutangaza kurejea tena CCM.
Sumaye ambaye wakati wa vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 alikihama Chama Cha Mapinduzi na kujiunga na Chama cha upinzania cha Chadema, ametangaza kurejea CCM akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally kwenye Kikao Maalum cha Baraza la Wadhamnini wa CCM.
Mapema Desemba 4, 2019 Sumaye alitangaza kuondoka Chadema na akisema anapumzika kufanya shughuli za siasa na kwamba atabaki kuwa mshauri kwa Chama chochote cha siasa kitakacho hitaji ushauri wake.
Akizungumza wakati huo, Sumaye alisema kwamba alikosea kujiunga na Chadema akisema kwamba alikwenda huko akidhani kuwa ndiko kuna Demokrasia zaidi kumbe sivyo.
Post a Comment