Katibu wa mabaraza huru ya wazee Ernest Bigirwamungu akizungumza na wananchi
Mzee Josephat Bombo akiipongeza juhudi za serikali
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani Muleba Athuman kahara (wapili kushoto) akikabidhi vitambulisho vya matibabu bure kwa baadhi ya wazee hao.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani Muleba Athuman kahara (wapili kushoto) akikabidhi vitambulisho vya matibabu bure kwa baadhi ya wazee hao.
Na Lydia Lugakila-:Kagera
Wazee wilayani Muleba mkoani Kagera wamemlilia Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli wakiomba itungwe sheria kutokana na sera ya taifa ya wazee ya 2003 ikiwemo kughulikiwa katika suala la pensheni.
Wazee hao wametoa kilio hicho katika hitimisho la maadhimisho ya miaka 43 ya kuzaliwa kwama cha mapinduzi CCM yaliyofanyika wilayani Muleba mkoani Kagera yaliyoendana na ugawaji wa vitambulisho vya matibabu bure kwa Wazee hao.
Bi theopist Leonard ni katibu wa wazee katika kata ya Mushabago wilayani humo ameipongeza serikali kushiriki pakubwa katika kuwahudumia wazee hao kwa kuwapatia stahiki zao ambapo serikali imeliangalia kwa umakini suala la vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee hao huku akimuomba Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuwasaidia kutungwa sheria kutokana na sera ya taifa ya wazee ya mwaka 2003 pamoja na suala la pensheni ambalo limekuwa likiwakosesha usingizi kila kukicha.
BI theopista ameishukuru serikali kwa namna ambavyo inawahudumia wananchi wake katika masuala ya ki maendeleo na kuongeza kuwa mwanzoni kundi hilo limekumbana na changamoto nyingi ikiwemo kunyanyaswa na baadhi ya watu wasio wema ambao wamekuwa wakiwaita washirikina, na kusukumwa wakiwa katika kufuata huduma ya matibabu huku wakiambiwa muda wao wa kuishi umekwisha.
Amesema baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani heshima kwa wazee hao imerudi ambapo changamoto mbali mbali zimetatuliwa.
Josephat Bombo mwenye umri wa miaka 79 ameishukuru serikali kwa juhudi kubwa zinazoelekeza mafanikio kwao lakini akataja kuwa wazee hao watapata usingizi endapo watashughulikiwa katika kupewa pensheni kwa wazee wote kama ilivyo kwa Zanzibar.
Aidha shirika la kwa wazee Nshamba kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya hiyo tayari wametekeleza maagizo ya serikali ya chama cha mapinduzi yanayoelekeza kila mzee mwenye umri wa miaka 60 na kuendelea ni lazima kupewa kitambulisho cha matibabu Bure.
Akikabidhi vitambulisho kwa wazee hao Mgeni rasmi katika sherehe hizo za miaka 43 ya kuzaliwa CCM mwenyekiti wa chama chama cha mapinduzi Wilayani Muleba Athuman Kahara amewataka wazee hao kuvitunza vitambulisho hivyo kwani vitasaidia kupata madawa kwa wakati tofauti na kipindi cha nyuma huku akiwahimiza wahudumu wa sekta ya afya kuweka ukaribu na kundi hilo hasa pale wanapofuata huduma hiyo.
Kahara ametoa pongezi kwa shirika la wazee Nshamba Wilayani Muleba chini ya Mratibu wake Lydia Lugazia kwa kazi kubwa ya kuwaunganisha wazee na kuwapatia huduma stahiki.
Elnest Bigirwamungu ni katibu wa mabaraza huru ya wazee Wilayani humo kupitia shirika la kwa wazee Nshamba amesema wazee 526 wamekwisha tambuliwa katika kata ya Mushabago ambapo jumla ya wazee waliopigwa picha na kupewa vitambulisho ni 513 na wazee 13 wakisubiria vitambulisho vyao.
Bigirwamungu amesema wazee 29,000 elfu walibainika kutoka katika kata 41 kati ya wazee 43 kwa wilayani hiyo ambayo imekwisha kuunda mabaraza huru ya wazee.
Ameongeza kuwa changamoto ambayo inawasumbua wazee ni pamoja kutoshirikishwa katika ngazi za vyombo vya maamuzi ikiwemo Kamati ya maendeleo ya kata, kijiji, baraza la madiwani hata Bungeni.
Hata hivyo katibu huyo ametoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuwaweka wazee katika Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kwani mchango wa serikali umewapa nguvu kubwa na matumaini ya kuishi.
Ikumbukwe kuwa vitambulisho hivyo vinatolewa kwa wazee wote waliotimiza miaka ,60 na kuendelea bila ubaguzi wowote.
Post a Comment