Ndugu Wanachama na watoa huduma wa Afya ya Kinywa na Meno. Hapa kwetu Tanzania kama ilivyo nchi zingine za Africa mashariki virusi hivi bado havijaingia ...Hata hivyo lazima tukumbuke kuwa, Dunia ya leo ni kijiji...Hivyo lazima tujipange na kujihadhari kwa maambukizi ya COVID-19 na kusambaa kwake.
Kwa sisi madaktari na wahudumu wa afya ya kinywa na meno tujikumbushe yafuatayo:
1. Kama ilivyo ada tuendelee kutumia vikinga maaambukizo kama mask, gloves, mawani, nk wakati tunahudumia wagonjwa wetu.
2. Tunawe mikono kabla
Na baada ya kuona mgonjwa kwa kutumia elbow corks ( zisizoshikwa na viganja vya mkono)
3. Kama inawezekana kutumia disinfectant soap inayomiminwa kutoka kwenye dispenser pump ni vema. Pia hand sanitizer zinaweza kutumika.
4. Tunawe mikono kabla ya kuvaa gloves, tunawe mikono baada ya Kuvua gloves .
5. Ikiwezekana tutumie hand tissues kukausha mikono yetu baada ya kunawa au air dryers.
6. Kila baada ya mgonjwa tubadilishe Mask na miwani ya kujikinga isafishwe na dawa za kuuwa vijidudu.
7. Baada ya kila mgonjwa kuonwa, dental chair na accessories zisafishwe na disinfectant kabla mgonjwa mwingine hajakaa.
8. 3 way syringes, hand pieces zibadilishwe au zisafishwe na kuwekewa vifuko maalumu/disposable covers
9. Burs na reamers zibadilishwe kwa kila mgonjwa
10. Dental aprons/bibs kwa kila
Mgonjwa.
11. Mgonjwa atumie mouth wash kabla ya matibabu , wakati wa matibabu ikihitajika , na baada ya matibabu.
12. Chumba cha matibabu kiwe
Na mzunguko wa hewa wa kutosha.
Tanzania Dental Association
Post a Comment