Featured

    Featured Posts

DC MJEMA:WANANCHI ACHENI 'KUWAVURUGA' WAKANDARASI

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza katika kkao cha Manispaa ya Ilala, kuwakabidhi wakandarasi miradi ya ujenzi wa madaraja ya Ulongon A na B jimboni Ukonga katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Anatpglou, Dar es Salaam juzi. Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mwita Waitara na Meya wa Ilala, Omary Kumbilamoto. Picha na Richard Mwaikenda.
Baadhi ya wadau wakisikiliza kwa makini wakati DC Mjema akizungumza.


Na Richard Mwaikenda

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewataka wananchi kuacha tabia ya kuwaingilia wakandarasi wanapotimiza wajibu wao katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amesema kinachotakiwa ni kujenga ushirikiano na wakandarasi na endapo wana ushauri mzuri ni bora wakaupeleka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ili aufanyie kazi.


"Wananchi mna haki ya kutoa ushauri na maoni kuhusu maendeleo ya ujenzi wa miradi, lakini msiwe chanzo cha kuchelewesha kukamilika kwa miradi, bali toeni ushirikiano hasa katika kufanikisha ujenzi,"amesema Mjema katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wakandarasi wa miradi hiyo pamoja na maofisa wachache wa Manispaa ya Ilala.

Mjema amezungumza hayo wakati wa kikao cha Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, cha kukabidhi kwa  wakandarasi miradi miwili ya ujenzi wa madaraja ya Zimbili/Ulongoni A na Ulongoni B katika Mto Msimbazi yaliyozolewa na mafuriko.

Makabidhiano hayo yaliyoongozwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara, awali yalipangwa yafanyike eneo la ujenzi, lakini hayakufanyika baada ya Serikali kupiga marufuku mikusanyika ya watu kutoka na kuzuka ugonjwa wa Corona.

Makabidhiano hayo yalihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Jumanne Shauri, Meya wa Manispaa, Omary Kumbilamoto pamoja na Mhandisi wa Ujenzi wa Mradi wa DMDP, Mhandisi John Magori.

Baada ya makabidhiano ya miradi hiyo, Waitara ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga iliyopo miradi, aliondoka na baadhi ya viongozi hao kwenda kukagua  maandalizi ya ujenzi wa miradi hiyo.

Alipofika eneo la ujenzi wa Daraja la Zimbili/Ulongoni A, Waitara alikuta mafundi wakiendelea na ujenzi wa kivuko cha muda cha watu, Bodaboda na Bajaji. Pia alipata wasaa wa kuwaeleza wananchi wachache waliokuwepo kufuata maelekezo yote yanayotolewa na serikali kuepukana na maambukizi ya Corona.

 Daraja la Zimbili/Ulongoni A litakalogharimu zaidi ya sh. bil. 4, litajengwa na Kampuni ya Chonqging International Corporation . Daraja la Ulongoni B pamoja na kipande cha barabara cha Km 7.5 litajengwa na Kampuni ya China Railway Seventh Group kwa gharama ya zaidi ya sh. bil. 17. miradi hiyo yote inatakiwa ikamilike ndani ya miezi 10.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana