Featured

    Featured Posts

GONJWA LA CORONA LAZIMA UHAI WA MWANAMUZIKI AURLUS MABELE, NCHINI UFARANSA

Mwanamuziki wa miondoko ya Soukous Aurlus Mabele (Pichani), amefariki Dunia nchini Ufaransa akiwa na miaka 67 baada ya kuugua kiharusi kwa muda mrefu na kisha kupata maambukizi ya virusi vya Corona hivi karibuni.

Rafiki yake wa karibu Nyboma Mwandido amethibitisha Aurlus Mabele kufariki dunia, huku taarifa zikieleza kuwa nguli huyo wa miondoko ya Soukous alifariki usiku wa kuamkia Ijumaa Machi 20, 2020.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa mwanamuziki huyo pia alikuwa akisumbuliwa kwa ugonjwa wa saratani ya koo, kwa miaka mingi, kabla ya kupata maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona.

Ugonjwa huo ambao ulianzia Wuhan nchini China na kusambaa katika nchi mbalimbali duniani, umeua zaidi ya watu 371 nchini Ufaransa.

Aurlus Mabele Alizaliwa mnamo mwaka wa 1953 huko Congo-Brazzaville katika wilaya ya Poto-Poto nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mwanamuziki huyo nguli ambaye jina lake halisi ni Aurélien Miatsonama, ambaye alianzisha kundi liitwalo "Ndimbola Lokole" alikuwa mmoja ya waanzilishi na lijendi aliyewahi kuanzisha kundi la Loketo akiwa na wanamuziki wenzake nguli kama Mav Cacharel na Diblo Dibala miaka ya 1980 japo baadae kundi lao lilivunjika.

Mabele akiwa na Mav Cacharel na Diblo Dibala walitengeneza muziki maarufu wa soukous ambapo baadaye akatajwa kama mfalme, na kupelekea msemo wa kuwa "Aurlus Mabele ndiye mfalme wa soukous".

Mwanamuziki huyo alikuwa ni msanii pekee aliyeweka makazi yake jijini Paris Ufaransa na kutamba katika miaka ya 1980 akitumia santuri.

Katika miaka 25 ya kazi zake ameuza zaidi ya nakala milioni 10 za albamu dunia nzima na alisaidia kwa kiasi kikubwa katika kuitambulisha na kuusukuma vilivyo muziki wa soukous nje ya mipaka ya bara la Afrika.

Japokuwa alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza kwa miaka mitano, lakini aliweza kujipanga ili kufanya matamasha na kundi zima la Loketo huko Ulaya kati ya mwezi Mei na Juni, 2009.

Kwa kushirikiana na wapiga magitaa maarufu na wenye vipaji, alitengeneza dansi ya Kiafrika yenye ladha yake ya kipekee ya soukous kwa kutunga nyimbo kama, Ivorian woman, Embargo, Betty De Asta, Evelyne, Africa Mousso, Femme ivoirienne», Loketo na Waka Waka.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana