Featured

    Featured Posts

IGP SIRRO TUMEJIPANGA KUKABILIANA NA UHALIFU


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema Jeshi la Polisi limejipanga vizuri katika kuhakikisha linakabiliana vyema na matukio ya uhalifu yanayojitokeza nchini na kwamba Jeshi lipo imara hasa kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

IGP Sirro amesema hayo wakati akikamilisha ziara yake ya ukaguzi katika Kanda Maalum ya Polisi Jijini Dar es salaam kwa kutembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia, ambapo amewataka askari wa vyeo mbalimbali kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria.

Kuhusu Corona, IGP Sirro amesema kuwa, Jeshi la Polisi limechukua hatua madhubuti ikiwemo kutoa elimu kwa askari wa vyeo mbalimbali na wateja wanaofika kupata huduma katika vituo vya Polisi kuhusu kujikinga ili kuendelea kudhibiti kusambaa kwa maambukizi ya ugonjwa wa corona.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana