Featured

    Featured Posts

RAIS MAGUFULI ATOA SH. BILIONI 15 KUMALIZIA UJENZI HOSPITALI YA MWALIMU NYERERE, MARA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu(kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima wakati walipokutana mkoani Marawakati Mawaziri hao walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo mkoani Mara

Na Mwandishi Wetu, Musoma.
Rais Dk. John Magufuli ametoa Sh. Billioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa hospitali ya Rufani ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyojengwa mkoani Mara kwa miaka 40 sasa bila kumalizika.

Haya yamebainika wakati wa ziara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi katika hospitali hiyo kujionea maendeleo ya ujenzi wake.

Akizungumza baada ya kutembelea Hospitali hiyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Hospitali hiyo itakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Mara hasa kwa huduma za matibabu ya kibingwa.

"Kutakuwa hakuna haja ya kwenda Hospitali ya Kanda Bugando kupata matibabu ya kibingwa kwani tunataka huduma za kibingwa zitolewe hapa hapa, "alisema

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa Shirika la Nyumba na Chuo Kikuu cha Ardhi kimepewa kazi ya kusimamia ujenzi wa Hospitali hiyo hivyo ameagiza kazi kufanyika usiku na mchana ili limalizike kwa muda uliopangwa.

"Tumekubaliana tarehe 17 mwezi huu wa tatu wawe wamekamilisha Wing C ili huduma za Mama na mtoto zinanze kutolewa kwa muda husika" alisema

Kwa upande wake Mkuu Mkoa wa Mara Adam Malima amemshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia hospitali hiyo iliyokwama kwa muda wa miaka 40 mpaka sasa.

“Hospitali hii imechukua awamu tano za marais kumalizika na tunamshukuru Rais kwa kuchukulia kipaumbele katika hili” alisema
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana