Featured

    Featured Posts

WAZIRI KAMWELWE AITAKA LATRA KUCHUKUA HATUA KUKABILIANA NA CORONA KWENYE VITUO VYA MABASI,ATOA SIKU TATU KUHAKIKISHA ZINARATIBU AGIZO HILO


Charles James, Globu ya Jamii

SERIKALI imeziagiza Halmashauri za Majiji na Miji kukaa na Mamlaka za Udhibiti Usafiri wa Ardhini (LATRA) ili kuweka utaratibu maalum ambao utadhibiti mrundikano na wingi wa watu kwenye vituo vikuu vya mabasi.

LATRA na Halmashauri hizo zimepewa siku tatu kuhakikisha zinaratibu agizo hilo ikiwa ni hatua za serikali katika kujikinga na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema wadau wote wa usafiri kwa kushirikiana na wataalamu wa afya na Shirika la ViwangoTanzania (TBS) wakae pamoja ili kuangalia njia gani watakazotumia katika kudhibiti wingi wa abiria vituoni.

Mhandisi Kamwelwe pia amewataka madereva na makondakta wa mabasi ya mijini kutekeleza kwa vitendo maelekezo watakayopewa juu ya idadi ya abiria wa kusimama kama itakavyoshauriwa na wataalam.

" Mamlaka hizo pia zinatakiwa kutenga vyumba maalumu kwa ajili ya abiria watakao bainika kuwa na dalili hizo ili vyumba hivyo viweze kutoa huduma ya kwanza huku taratibu nyingine za kuwafikisha sehemu ya tiba zikifanyika", Ameagiza Waziri Kamwele

Kuhusu usafiri wa Treni, Mhandisi Kamwelwe ameliagiza Shirika la Reli Nchini (TRC), lile la Tanzania na Zambia (TAZARA) Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) kuweka vitakasa mikono kwenye vyombo vyao vyote vya usafiri ikiwa ni agizo la Waziri wa Afya katika kukabiliana na mamabukizi hayo.

Mhe Kamwelwe pia ametoa wito kwa mamlaka hizo kushirikiana na wataalam wa afya katika kutoa elimu kwenye vituo vya mabasi, bandari, kwenye vivuko, uwanja wa ndege na kwenye stesheni ili kuwasaidia wananchi ambao ndio wasafiri kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana