Featured

    Featured Posts

CAG ABAINI KUWEPO KWA ONGEZEKO LA DENI LA SERIKALI KWA BOHARI KUU YA DAWA

Charles James, Michuzi TV

RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Nchini (CAG) kwa mwaka ulioisha Juni 2019 imebaini kuwepo kuongezeka kwa deni la serikali kwa bohari kuu ya dawa (MSD) kwa kiasi cha Sh bilioni 16.18 kutoka Sh bilioni 37.48 za mwaka uliopita.

Ukaguzi huo wa CAG una mashaka kuwa ukwasi wa MSD unazidi kushuka hivyo kuathiri utekelezaji wa mipango mbalimbali ikiwemo usambazaji wa dawa na vifaa tiba kwa jamii pamoja na utekelezaji wa mipango yake mingine.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma, CAG Charles Kichere amesema pia amebaini kuwa Shirika la TTCL liliingia mkataba na Kampuni ya MIC Tanzania kwa ajili ya kupitisha mawasiliano yake kitaifa kuanzia Julai 14, 2018. Dhumuni likiwa kuongeza mapato.

Kichere amesema alibaini TTCL ilikua ikitoza bei rahisi kwenye vifurushi inavyouza kwa wateja wake kuliko bei inayolipa kwa mujibu wa mkataba jambo ambalo limesababisha shirika hilo lipate hasara ya Sh bilioni 1.11 katika mkataba huo wa kupitisha mawasiliano pekee.

Amesema kama TTCL itachukua hatua ya kuongeza bei ili kupunguza hasara kuna uwezekano wa kupoteza mapato kutokana na ushindani uliopo katika soko.

CAG Kichere pia amebaini upotevu wa malipo yasiyo na tija kwa watumishi waliokua watumishi wa mashirika ya umma fedha sh milioni 829.45 kwa watumishi waliocha kazi na kuhama.

" Nilibaini kuwa mashirika ya umma matatu yalilipa malipo mbalimbali yenye jumla ya sh milioni 829.45 kwa watumishi walioacha kazi au kuhama kwa sababu mbalimbali. Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB) ililipa kiasi cha Sh milioni 398.14, Mamlaka ya Udhibiti wa Mbelea Tanzania (TFRA) ililipa Sh milioni 324.01. Na Mamlaka ya Bandari (TPA) iliripoti mikopo ya Sh milioni 107.30 ambayo ilitolewa kwa watumishi walioacha kazi.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) ililipa Sh bilioni 1.58 kama posho za mwezi wa ziada kinyuma na kanuni za kudumu kwa watumishi wa umma zinazotaka mtumishi kupewa posho ya kusafiri wakati wa likizo mara Moja kila baada ya miaka miwili. Hali hii imesababisha hasara na matumizi mabaya ya fedha za umma," Amesema Kichere.

Amesema pia amebaini kuwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii na bima za afya zina madai makubwa ambayo ni chechefu, mengi ya madeni hayo ni kwa serikali na taasisi zake. Mpaka kufikia Juni 2019 mifuko hiyo ilikua ikiidai serikali pamoja na taasisi zake Sh trilioni 2.42.

Aidha wakati wa uhakiki wa madeni ya Shirika la Uzalishaji Umeme Tanzania (TANESCO) aliomba uthibitisho wa madeni ya toka kwa wadeni ambapo ni Kampuni 23 pekee ndizo zilizoweza kuthibitisha madeni yao yenye thamani ya Sh bilioni 647 huku kampuni 913 zenye madai yenye thamani ya Sh bilioni 291 hazikuthibitisha madeni yao.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG, Charles Kichere akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokua akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ripoti yake kwa mwaka ulioisha Juni 2019.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana