Tarehe 21 Aprili ilikuwa siku ya kutimiza umri wa miaka 94 kwa Malkia Elizabeth II.
Kwa kawaida mtawala wa Uingereza anasherehekewa siku ya kuzaliwa mara mbili kila mwaka.
Moja ni siku yake halisi ya kuzaliwa, na nyingine ni siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Malkia iliyowekwa na serikali.
Kutokana na hali mbaya ya maambukizi ya virusi vya Corona, malkia Elizabeth ameamua kufuta sherehe za kutoa heshima ya mizinga mwaka huu.
Post a Comment